Categories
Afya ya mwanamke na uzazi Siku za hatari

Je Unaweza Kushika Mimba Kwenye Hedhi?

kushika mimba kwenye hedhi
Upt

Endapo unatafuta mimba kwa muda mrefu bila mafanikio au unataka kushika mimba haraka, ni muhimu kufatilia kwa makini mzunguko wako wa hedhi kujua zipi siku za hatari. Moja ya imani potofu sana kwa wengi ni kuamini mwanamke hawezi kushika mimba kwenye hedhi.

Japo uwezekano ni mdogo wa kushika mimba wakati wa hedhi lakini inawezekana. Hapa chini ni maelezo ya kina unayotakiwa kufahamu kuhusu kufanya tendo na kushika mimba wakati wa hedhi.

Mimba inatungwaje?

Mchakato wa kushika mimba kwa mwanamke ni moja ya maajabu makubwa sana ya uumbaji wa binadamu. Yahitaji mbegu kutoka kwa mwanaume iungane na yai kutoka kwa mwanamke.

Yai likishapevuka na kutolewa kutoka kwenye mfumo wa mayai, linaweza kushi kwa masaa 12 mpaka 48 kabla ya kuharibika. Mbegu ya amwanaume ikishatolewa inaweza kuishi ndani ya kizazi cha mwanamke kwa siku mpaka tatu mpaka tano.

Siku za hatari

Wanawake wengi hupata hedhi kila baada ya siku 28 mpaka 33 za mzunguko. Na wengi wao mayai hukomaa siku ya 14 baada ya hedhi . Siku yai kutolewa inaweza pia kuwa ya 12, 13 14 au 15, siku hizi ndizo tunaziita siku za hatari.

Kitendo cha yai kupevuka na kutolewa kwa ajili ya urutubishaji huitwa ovulation. Na endapo kama yai na mbegu vitakutana basi uwe na uhakika mimba itatungwa.

Nini kinapelekea kushika mimba kwenye hedhi?

Siku ya yai kupevuka na kutolewa inatofautiana kulingana na mzunguko wako. Baadhi ya wanawake wenye mzunguko mrefu wa siku mpaka 35, ovulation yaweza kutokea siku ya 21 . Na wanawake wenye mzunguko mfupi zaidi wanaweza kushika mimba hata siku ya 7 ya hedhi.

Sasa kwa mantiki hii, chukulia hedhi yako inachukua siku 6 kuisha. Umefanya mapenzi na mtu katika siku ya tano ya hedhi, na yai ikapevuka siku ya 7, na tunajua mbegu zinaweza kukaa siku mpaka 6 ndani ya kizazi. Maana yake unaweza ukashika mimba ukikutana na mwanaume kwenye siku za hedhi yako.

Sababu ingine ni kuchanganya bleed ya ovulation na bleed ya hedhi.

Wakati wa ovulation mwanamke anaweza kupata matone kidogo ya damu kwa siku moja . Wanawake wengi waaweza kuhisi ni damu ya hedhi. Kufanya tendo bila kinga katika muda huu utaweza kushika mimba.

Kama unahitaji kufatilia vizuri kujua siku zako za hatari, anza kwa kuweka rekodi ya mizunguko yako ya hedhi kwa miezi walau mi4. Andika lini unaanza hedhi, unamaliza baada ya muda gani, hedhi yako ikoje?.
Ukifatilia kwa miezi kadhaa ni rahisi kujua siku zako za hatari na ukaweza kucheza salama.

Uwezekano ukoje wa kushika mimba kwenye hedhi?

Chansi ya kushika mimba kwa mwanamke unaongezeka na kupungua kulingana na mwenendo wa siku zako za yai kupevuka. Uwezekano wa kushika mimba siku ya kwanza na ya pili ya hedhi ni mdogo sana chini ya asilimia 1.

Baada ya kuanza hedhi kwenye siku ya 13 uwezekano wa kushika mimba ni karibu asilimia 9 na chansi kuongezeka zaidi siku ya ovulation.

Tumia uzazi wa mpango kuepuka kushika mimba kwenye hedhi

Endapo bado hujajiandaa kabisa kushika mimba unaweza kuamua kutumia uzazi wa mpango. Nenda hospitali, onana na daktari atakupa maelekezo ya njia zote zinazopatikana ikiwemo faida na hasara za kila njia ya kupanga uzazi.

Baada ya maelezo ya daktari, utaweza kuchagua njia sahihi ya kutumia itakayokufaa ili kuzuia kushika mimba kwenye hedhi. Kumbuka tu kwamba njia nyingi za uzazi wa mpango haziwezi kukuzuia kupata magonjwa ya zinaa.

Zitakukinga tu dhidi ya miba isiyotarajiwa. Kama huna uhakika na mwenzi wako, hakikisha unatumia kinga kama kondomu, itakusaidia kukukukinga na magonjwa ya zinaa na mimba pia.

Hitimisho

Mzunguko wa hedhi unatofautiana kwa kila mwanamke, hivo inawezekana kabisa ukashika mimba siku za hedhi. Japo chansi ya kushika mimba ni ndogo mwanzoni mwa hedhi ila kadiiri unavokarbia siku ya ovulation chansi inaongezeka.

Kama umeshajaribu kutafuta mimba kwa zaidi ya mwaka mmoja bila mafanikio, muone daktari kupata vipimo na tiba. Daktari anaweza kukwelekeza vizuri namna ya kufatilia siku za hatari ili ushike mimba mapema.
Daktari pia anaweza kukufanyia vipimo kadhaa na kukupa dawa za kuchochea upevushaji wa mayai na kuongeza chansi ya kushika mimba.

Unahitaji maoni na Ushauri? Tuandikie kwa Whatsapp namba 0678626254. Usipige simu namba ni ya whatsapp tu

Bofya kusoma makala inayofuata: Jinsi ya kugundua siku za hatari kushika mimba

Categories
Tendo la ndoa

Tendo la Ndoa wakati wa Ujauzito

tendo la ndoa wakati wa ujauzito
mjamzito

Kama mwanamke unaweza kuwa unanjiuliza kama ni salama kufanya tendo la ndoa wakati wa ujauzito ama siyo salama.

Pengine unafikiri yaweza kupekea mimba kuharibika? Au mtoto kupata majeraha? Pengine wajiuliza kuna staili fulani za tendo ambazo ni salama zaidi kwa mjamzito? Hapa chini ni taarifa muhimu ambazo watakiwa kuzifahamu.

Je Kufanya Tendo la Ndoa Wakati wa Ujamzito Ni Salama?

Jibu ni ndio, kufanya tendo wakati wa ujauzito ni salama kabisa. Uume kuingia ndani ya uke,zile pilika za kuingiza na kutoa haziwezi kuathiri mtoto, kwa sababu analindwa na tumbo na misuli ya ukuta wa kizazi pia.

Lakini pia mtoto analindwa na majimaji mazito(amniotic fluid).
Usijali kuhusu kusinyaa na kutanuka kwa uke pale unapofikia kilele, hakuwezi kufanya mimba ikatoka. Kutanuka huku ni tofauti na wakati wa kuzaa.

Mazingira gani inashauriwa usifanye tendo la ndoa wakati wa ujauzito?

Daktari anaweza kushauri usifanye tendo la ndoa kama

  • una historia ya mimba kuharibika mara kwa mara
  • uko kwenye hatari ya kupata uchungu mapema kabla ya week 37 za ujauzito
  • unatokwa na damu na maumivu yasijulikana sababu yake
  • chupa imepasuka na maji yanavuja
  • mlango wa kizazi umefunguka mapema zaidi
  • una tatizo kitaalamu placenta previa yani tishu za mirija unaomlisha mtoto chakula na hewa safi, umekuwa mpaka kuziba mlango wa kizazi
  • kama unatarajia kujifungua watoto mapacha

Je naruhusiwa kupiga punyeto badala ya tendo?

Fahamu kwamba daktari akishauri usifanye tendo anamanisha pia usifanye kitu chochote ambacho kinakuamsha hisia na kukufikisha kileleni mfano kutumia dildo an vidole/ kupiga punyeto.

Hamu ya Tendo la Ndoa wakati wa Ujauzito

Kila mwanamke mwanamke mjamzito anatofautiana namna anavojisikia kuhusu tendo. Baadhi hamu ya tendo hupotea kabisa. Wengine hufurahia zaidi tendo na kupata msisimko zaidi wa mapenzi wakati huu.

Kipindi cha ujauzito ni kawaida kwa hamu ya tendo kubadilika. Muhimu zungumza na mpenzi wako namna unavojisikia. Mueleze unapenda staili ipi nzuri ya kufanya tendo isiyokuumiza.

Staili za Kufanya Tendo Kwa Mjamzito

Baada ya miezi minne ya mimba,usifanye tendo kwa njia ya kawaida ya baba na mama kwa kulala kitandani na mme wako akaja kwa juu. Itakusaidia kuepuka changamoto za mzunguko wa damu..

Staili nzuri ya kufanya tendo ni kwa wote kulala kwa ubavu. Kisha mwanaume akaingiza uume kwenye uke kupitia nyuma yako na pia dogie style,yani mwanamke kupiga magoti na mwanamume kuingiza uume kwa nyuma.

Kama huna uhakika na mwanaume unayekutana nae kipindi hiki cha ujauzito basi hakikisha anavaa kondomu. Kuwa na mimba haizuii kutoambukizwa magonjwa ya zinaa kama ukimwi, kisonono na chlamydia-maana maambukizi haya huathiri mtoto moja kwa moja.

Tendo la Ndoa Baada Ya Kujifungua

Kwa week 6 za mwanzo baada ya kujifungua inashauriwa usifanye tendo la ndoa. Sababu zikiwa unahitaji:-

  • kupona kidonda wendapo njia ya uke ilikatwa kidogo kuongeza mlango wa mtoto kutoka
  • kupona kidonda cha tumbo endapo kama ulijifungua kwa upasuaji
  • uchovu kutokana na kujifungua
  • mabadiliko ya homoni yatapelekea ukose hamu ya tendo kwa muda
  • baaada ya kuzaa ni kawaida kuendelea kupata bleed kwa week 4 mpaka 6
  • Stress kutokana na kuwaza sana kuhusu majukumu mapya kama mzazi

Kwa ujumla tendo la ndoa lifanyike baada ya mama kupona kabisa. Ongea na daktari wako akupe ushauri lini itakuwa sawa. Kwa kiasi kikubwa week 6 zinafaa kusubiri kabla ya kuanza tena tendo la ndoa. Muhimu hakikisha tu una utulivu kihisia na kimwili kabla ya kuanza .

Bofya kusoma makala inayofuata: Bawasili kwa mjamzito, Ushauri na tiba