
Bilashaka umewahi kusikia kuhusu kisukari cha mimba. Kama una maswali zaidi kuhusu tatizo hili na unataka kujua nini cha kufanya kupunguza hatari basi makala hii ndio kila kitu kwako.
Nini maana ya kisukari ha mimba yani Gestational diabetes?
Okey hiki ni kisukari anachopata mjamzito pale ambapo kiwango cha sukari kwenye damu kinapanda sana , na mwili wako hauzalishi insulini ya kutosha kupunguza ile sukari.
Kuna makundi mawili ya kisukari ya mimba. Kundi la kwanza tuite class 1 hii inaweza kudhibitiwa kwa kurekebisha tu vyakula na mtindo wa maisha, na kundi la pili tuite class 2 hii itahitaji upate matibabu ya dawa hospitali.
Ukicha kile kisukari ha ukubwani ambacho wanaugua watu wengi, hiki kisukari cha mimba kinampata mtu pale tu akiwa mjamzito na kwa wanawake wengi wanapona baada ya kujiungua.
lakini tafiti inaonesha pia kwamba unakuwa kwenye hatarri ya kuugua kisukari cha ukubwani pale ukiwa na kisukari cha mimba.
Je nini kinapalekea mwanamke kuugua kisukari cha mimba?
Wakati a mimba, kondo yani placenta inaweza kuzalisha vichocheo ambavyo vinapeleka sukari kuwa nyingi kwenye damu na kupelekea kiasukari cha mimba. Baada ya mtoto kuzalishwa na kondo kutolewa sukari inarudi kawaida.
Dalili za kisukari cha mimba
Kisukari ha mimba gestational diabetes chaweza kupelekea dalili kama
- mdomo kukauka
- kukojoa mara kwa mara
- kuhisi mwili kuchoka sana
- kuhisi kiu kuliko kawaida
Je tatizo ni kubwa kiasi gani??
Japo kiwango cha wanawake wanaogundulika kuwa na kisukari cha mimba ni ndogo, karibu 10% ya wanawake duniani wanapata shida hii kwa mwaka.
Madaktari pia wanajua kwamba baadhi ya sababu zinachangia kuwa kwenye hatari zaidi kama
Umri: Tafiti zinasema wanawake wenye zaidi ya miaka 30 wanapata zaidi tatizo.
Uzito: Wenye uzito mkubwa na kitambi wapo kwenye hatari mara 3 ya kuugua.
Historia kwenye familia: Kama kwenye familia yako kuliwahi kutokea wagonjwa wenye kisukari cha mimba, basi na wewe utakuwa kwenye hatari ya kupata shida hii.
Je lini unatakiwa kupima kujua kama una kisukari cha mimba?
Kipimo kwa kiasi kikubwa kinafanyika kati ya wiki ya 24 mpaka 28 kwenye mimba. Wajawazito waliopo kwenye kundi hatarishi ama wenye historia ya tatizo wao hupimwa mapema zaidi kwenye miezi mi3 ya kwanza.
Je nini ufanye ikiwa utajikuta unaumwa yani +ve?
Kama utakutwa na kisukari, usipaniki. Daktari wako atakuwa nawe bega kwa bega kuhakikisha unapata matibabu na ushauri sahihi kwa tatizo lako. Kumbuka unaweza kupona kwa lishe na maoeiz tu ndani ya muda mfupi. Hakikisha unauliza maswali yote ukiwa na daktari ili upate ufafanuzi wa kina.
Utaelekezwa kufatilia sukari yako kila siku kwa kupima. Kama sukari yako haiwezi kutibika kwa lishe na mazoezi, hapo utaweza kuanzishiwa dawa ambao ni salama kwa ujauzito wako.
Yapi madhaar ya Kisukari cha mimba?
Kisukari cha mimba chaweza kupekea matatizo kadhaa kama kuzaa mapema kabla ya mda, kujifungua mtoto mwenye uzito mkubwa zaidi kuliko kawaida na pia yaweza kuhitaji ujifungue kwa upasuaji. Hutakiwi kuogopa wanawake wengi wanapata hili tatio linaisha baada ya kuzaa na wanaendelea na maisha yao.