Categories
Uzazi wa Mpango

Njia asili za kupanga Uzazi

ufatiliaji wa mzunguko-kushika mimba
kupanga uzazi kupitia kalenda

Kwanini tunasema hizi ni njia asili-natural contracepives? Ni kwa sababu hazibadili mpangilio wa homoni au vichocheo kwenye mwili. Badala yake njia hizi zinamwongoza mke na mume kutofanya ngono wakati yai limepevuka.

Yani lengo ni kutoruhusu mbegu ikalifikia yai lililokomaa kurutubishwa. Ni muhimu sana kufatilia kwa ukaribu viashiria vyote vya yai kupevuka.

Kikawaida yai hutolewa kila baada ya siku 14 kabla ya hedhi ijayo. Hapo kwenye siku 14 toa siku mbili nyuma au ongeza siku mbili mbele. Lakini kwasababu yai linaweza kuishi mpaka siku 3 au 4 baada ya kutolewa na mbegu inaweza kuishi siku mbili mpaka tano, kufanya mahesabu vizuri inabidi uzingatie kwa week na siyo kwa siku.

Njia asili za kupanga uzazi zinafanya kazi kwa asilimia mpaka 98, lakini zinataka ufatiliaji wa kila siku na kujicontrol hisia zako.

Njia ya kwanza ni calender

Hii inawafaa zaidi wenye mzunguko mzuri. Ni topic ndefu inayohitaji kusoma taratibu na kuelewa. Ni zoezi ambalo laweza kuchukua miezi miwili mpaka mia4 kulifatilia na kulizoea, kwani yatakiwa kurekodi na kufatilia matukio na mabadiliko yote ya mwili wako.

Hatua kwa hatua za kufatilia kalenda

  1. Kwa miezi 8 mpaka 12, rekodi siku ambayo unaanza hedhi na uhesabu siku zote za kila mzunguko. Siku ya kwanza ni ile unayoanza hedhi katika mwezi husika na hesabu mpaka siku unayoanza hedhi katika mwezi mwingine hapo mzunguko mmoja utakuwa umekamilika
  2. Rekodi mzunguko mfupi na mzunguko mrefu zaidi katika ufuatiliaji wako. Kupata siku yako ya kwanza ya hatari, chukua namba ya mzunguko mfupi zaidi toa 18, mfano mzunguko wako mfupi ni siku 27-18 inabaki 9.
  3. Kupata siku yako ya mwisho ya hatari kwenye mzunguko, chukua siku za mznguko wako mrefu toa 11. Mfano mzunguko wako mrefu ilikuwa siku 30-11 inabaki 19.Katika mahesabu hapo juu ni kwamba siku kati ya mzunguko mfupi na mrefu ndizo siku zako za hatari, kwa maaana ya kuanzia siku ya 9 mpaka siku ya 19 ndizo siku zako za hatari.
  4. Kama unataka usishike mimba basi usifanye ngono siku ya 9 ya hedhi mpaka siku ya 19, au utumie condomu.

Kufatilia joto la mwili-Basalm metabolic rate.

Joto la mwanamke hushuka masaa 12 mpaka 24 kuelekea mda wa ovulation, baada ya hapo joto huongezeka tena baada ya ovulation. Tukisema ovulation maana yake muda wa yai kutolewa kwenye kikonyo chake na kuwa tayari kw aurutubishaji. Mabadiliko haya ya joto ni madogo sana chini ya nyuzi moja.

Kupima joto hili tumia kipimajoto maalumu kinachopatikana famasi, na upime kila siku asubuhi kabla ya kuamka. Kutumia joto la mwili kama njia ya kujua siku za hatari, mwanamke anatakiwa asifanye ngono kwenye siku ambazo joto linashuka. Utasubiri masaa 48 mpaka 72 baada ya joto kupanda ndipo ufanye tendo.

Kufatilia ute wa uzazi.

ute wa mimba

Njia hii ya ute inataka kufatilia mabadiliko ya uteute kwenye uke katika siku tofauti za mzunguko wako. Mwanamke atazalisha ute mwingi laini, unaovutika kama yai kwenye siku za hatari. Sasa wewe kama mwanamke unatakiwa ujifunze kufatilia na kutofautisha ute huo kwa kutumia vidole viwili. Ingiza ukeni taratibu kisha fanya kama unavuta kuona kama unavutika. Kama hutaki kushika mimba basi usifanye kabisa tendo kwa siku 3 mpaka 4 tangu uone huo ute ute wa kuvutika.

Ovulation Kits

kipimo cha kufatilia ovulation

Mwanamke anaweza kutumia vifaa malumu vya kufatilia yai kupevuka. Vifaa hivi vina mfanano na kipimo cha mimba cha mkojo ya UPT. Vipimo hivi vinaangalia kiwango cha homoni ya lutenizing(LH) kwenye mkojo. Homoni ya lutenizing inaongezeka masaa 20 mpaka 48 kabla ya ovulation. Vifaa vya kupima vinapatikana kwenye famasi, unaweza kununua package yako ukaweka ndani.

Utaanza kupima siku mbili mpaka tatu kabla ya siku ambazo unafikiri yai linakarbia kutolewa. Kipimo hichi kama ilivyo kwa kile cha UPT, kinapima mkojo na kunyesha rangi nyekundu. Kama yai limeshatolewa mistari mwili iliyokolea itatokea, na kama bado mstari utakuwa mmoja mwekundu. Kama ovulation imekaribia basi mstari utakuwa umepauka.

Vipimo hivi kwa kiasi kikubwa hutumika kufatilia yai kupevuka ili mwanamke aweze kushiriki apate mimba, lakini unaweza kuvitumia pia kupanga uzazi ili usishike mimba mapema wakati hujatarajia.

Withdraw method (kuchomoa uume kabla mbegu hazijatoka)

Withdraw inahitaji mwanaume kutoa uume haraka kabla mbegu hazijatoka wakati wa tendo. Changamoto ya njia hii ni kwamba wanawaume wachache wanaweza kujizuia na wakatoa uume nje kwasababu ya hisia kali na utamu wa kufika kileleni. Lakini pia mbegu kidogo zinaweza kutoka wakati mwanaume anakarbia kilele na zikasababisha mimba. Njia hii ina ufanisi wa asilimia 75 mpaka 80 katika kuzuia mimba.

Lactational infertility.

Njia hii inamaanisha kwamba unapokuwa unanyonyesha mayai yanakuwa hayapevuki kwahivo mimba haitaingia. Wanawake wanaonyonyesha, mayai huanza tena kupevuka week 10 mpaka 12 baada ya kujifungua. Katika miezi sita ya kwanza ambapo mtoto ananyonya pasipo kula chakula kingine, njia hii inakuwa na ufanisi zaidi.

Mtoto yatakiwa anyonye walau kila baada ya masaa ma4 na usipitishe zaidi ya masaa sita bila kumnyonyesha mtoto. Hakikisha unatumia njia hii miezi 6 tu ya mwanzo baada ya kujifungua. Faida zake ni kwamba huhitaji kutumia kinga yoyote wala njia yoyote ya kemikali ili kuzuia mimba,badala yake ni kunyonyesha tu ipasavyo.

Njia hii siyo ya uhakika kutumika pasipo kuzingatia njia zingine hasa baada ya miezi 6 kuisha na mtoto kuanza kula. Mwanamke anayenyonysha anaweza kushika mimba pale mtoto akipunguziwa ratiba ya kunyonya kwa siku.

Kuosha uke na kukojoa baada tu ya tendo

Njia hii inahitaji mwanamke kila anapomaliza tendo kwenda haraka washroom na kuchuchumaa kisha kunawa na kutoa mbegu na uchafu wote ukeni. Wanawake wengi pia husimama haraka na kukojoa ili mbegu zitoke nje kabla ya kulifikia yai. Njia hizi hazina uhakika hivo hakikisha unatumia na njia ingine kuzuia mimba.

Kutofanya kabisa tendo

Hapa mwanamke na mwanaume wanaweza kuamua kutokutana kabisa ili kuepuka mimba. Hii ndio njia pekee yenye uhakika wa asilimia mia kukukinga usishike mimba ambayo hujatarajia. Badala yake kila mmoja anaweza kufanya punyeto ili kujiridhisha.

Unahitaji maoni na Ushauri? Tuandikie kwa Whatsapp namba 0678626254. Usipige simu namba ni ya whatsapp tu

Categories
Uncategorized

Kiwango cha mayai ya mwanamke

yai la mwanamke

Mwanamke ana mayai mangapi?

Natambua una kiu sana ya kutaka kufahamu idadi ya mayai uliyonayo, na kama bado una uwezo wa kushika mimba kulingana na umri wako wa sasa. Makala hii itajibu maswal yako mengi kuhusu mayai ya mwanamke na uzazi.

Je watoto wa kike wanazaliwa na mayai?

Jibu ni ndio, watoto wa kike huzalishwa na mayai yote wanayotakiwa kuwa nayo. Hakuna mayai mapya yatazalishwa tena kwenye maisha yako kama mwanamke.

Mayai mangapi mwanamke anazaliwa nayo?

Pale kichanga kinapokuwa bado tumboni mwa mama kinakuwa na mayai karibu millioni 6. Mayai haya yanakuwa hayajapevuka na huitwa oocytes. Mpaka kufikia kuzaliwa mayai yanapungua mpaka milioni 1 mpaka 2.

Kwanini mtoto mdogo hapati hedhi wakati tayari ana mayai?

Hili ni swali zuri sana, kwamba nini sasa kinazuia mtoto asianze hedhi wakati tayai ana mayai? Mzunguko wa hedhi husubiri mpaka kipindi cha kubalahe ama kuvunja ungo. Balehe huanza pale ubongo unapoanza kuzalisha homoni ya GnRH-Gonatrophin-releasing hormone.

GnRH inachochea tezi ya pitutary ambayo huzalisha homoni ya FSH-follicle stimulating hormone. FSH ndio inachochea sasa mayai kuanza kupevuka.

Hedhi huanza kama miaka miwili baada ya matiti kuota. Wanawake wengi huvunja ungo na kuanza hedhi wakiwa na miaka 12 mpaka 15. Wachache sana huvunja ungo mapema wakiwa na miaka 8.

Mwanamke ana mayai mangapi anapovunja ungo?

Pale mwanamke anapofikia balehe, anakuwa na idadi ya mayai laki 3 mpaka laki 4. je nini kimetokea kwenye mayai mengine? Hili ndio jibu sahihi:- ni kwamba mayai mengi karibu 10000 yanakufa kila mwezi kabla ya balehe, yaani hayafikii kwenye kupevuka.

Mayai mangapi yanakufa kila mwezi baada ya mwanamke kuvunja ungo?

habari njema ni kwamba idadi ya mayai uanayokufa kila mwezi inapungua sana baada ya kuvunja ungo. Tafiti zinasema kwamba mwanamke anapoteza mayai 1000 kila mwezi baada ya kuanza hedhi/kuvunja ungo. Hii ni kama kusema unapoteza asilimia 30 mpaka 35 ya mayai kila mwezi.

Kila mwezi ni yai moja tu linapevuka na kuwa tayari kwa mimba kutunga kwenye siku za hatari. Ni mara chache sana inatokea mayai mawili yakawa tayari kwa kurutubishwa. Hapo ndipo wanapatikana mapacha wasiofanana.

Mwanamke ana mayai mangapi kwenye miaka ya 30s?

Mwanamke anapofikia miaka 32 uwezo wake wa kushika mimba unapungua sana na unashuka zaidi anapofika 37. Kuanzia miaka 35 mpaka 37 mayai yanakuwa chini ya laki 1. Hii ni sawa na kusema mayai yamebaki asilimia 3 tu ya hifadhi yote.

Mayai mangapi yanabaki kwa mwanamke wa miaka 40?

Pengine uko na miaka 40 na bado una kiu ya kushika mimba. Sasa unawaza umebakiwa na mayai kiasi gani. Tafiti zinasema kwamba kikawaida mwanamke anapofika miaka 40, idadi ya mayai inapungua chini ya 18,000/=. japo chansi ya kushika mimba iko chini, haimaanishi kwamba huwezi kushika mimba, bado inawezekana kubeba ujauzito katika umri huu.

Nini kinatokea baada ya kukoma hedhi?

Pale unapokoma hedhi na mayai kuisha, mifuko ya mayai inakoma kuzalisha homoni ya estrogen. Na hivo utaanza kupata dalili za tofauti kama ukavu ukeni, uchovu, kukosa hamu ya tendo. Endapo ulizaliwa na mayai mengi, kuna chansi kubwa ukaweza kushika mimba na ukapata mtoto hata kwenye miaka ya 40s.

Hitimisho

Umri mzuri wa kubeba mimba na kuzaa ni miaka ya 20s. Hapo ndipo mwanamke anakuwa na mayai ya kutosha na chansi ya kushika mimba ni kubwa sana. Kama unatafuta mimba kwa muda mrefu bila mafanikio, inahitaji uonane na daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake. Wote wawili me na ke mfanyiwe vipimo kujua chanzo cha tatizo.

Unahitaji maoni na Ushauri? Tuandikie kwa Whatsapp namba 0678626254. Usipige simu namba ni ya whatsapp tu

Unataka kusafisha kizazi na kuongeza uzalishaji mayai? bofya hapa upate dawa asili zenye ubora

Categories
Natural remedies

Hatua Tano za kusafisha meno kwa njia asili

kusafisha meno na kuwa na meno meupe
Kusafisha meno inachukua muda

Zaidi ya asilimia 18 ya watu hufisha meno yao wakati wa kupiga picha, wengi wakiogopa aibu ya kuonekana wan meno machafu. Kuwa na meno meupe ni jambo kubwa sana katika jamii yetu ya sasa. Leo nitakwelekeza hatua rahisi tano za kusafisha meno yako ukiwa nyumbani, bila kutumia dawa zenye kemikali.

Meno ya Kun’gaa ni kiashiria cha usafi

Meno yako ni kitu cha kwanza watu wanakiona wanapokutazama, ni kiashiria cha utimamu wa afya yako na chanzo chako cha kujiamini mbele za watu. Kuwa na meno ya rangi nyekundu au njano ni kiashiria kwamba hujali kabisa afya yako. Bilashaka unahitaji nawe kuwa na tabasamu mawanana mbele za watu bila kuogopa.

Baadhi ya watu, pamoja na kusafisha meno asubuhi, bado wanakuwa na utando kwenye meno. Hii ni kutokana na tabia kama za kunywa kahawa au chai na kuvuta sigara. Meno ya njano au kijivu yanaweza kuashiria tatizo kubwa zaidi la kiafya. Kusafisha meno pekee bado haitoshi kulinda afya ya kinywa, unahitaji na kurekebisha chakula unachokulana mtidno wako wa maisha.

Kwanini meno yanabadilika kuwa na wekundu ama njano?

Meno yanachafuka na kubadilika kuwa na wekundu , njano ama wakati mwingine kuwa na weusi, kwasababu ya kugandamana kwa uchafu. Pamoja na kwamba ni ngumu kwa meno kuwa na weupe ule ule miaka yote mpaka uzee, kuna sababu nyingi zinafanya meno kuchafuka na uanweza kuziepuka.

Sababu hizi ni kama

  • kunywa kahawa na chai nyeusi
  • kuvuta sigara
  • lishe mbovu ikiwemo vitu vya sukari, soda nk
  • tatizo la mdomo mkavu (mate husaidia kulinda meno)
  • kupumua kupitia mdomo na kuziba kwa njia za pua. Hali hii inapunguza kiwango cha mate mdomoni
  • matumizi ya antibitics kwa muda mrefu
  • matumizi makubwa ya vitu vyenye madini ya fluoride na
  • changamoto za kurithi

Njia asili za kusafisha meno yakawa na weupe

1.Brush meno baada ya kunywa ama kula

Njia nzuri ya kusafisha meno yako yawe meupe ni kupiga mswaki baada ya kumaliza kula ama kunywa. Japo siyo rahisi kufanya kila mara lakini inawezekana ukijizoesha. Inategemea pia na eneo ulilopo, aidha makazini ama shuleni, anza kwa kupiga mswaki kabla ya kulala. Fanya hilo zoezi kwa mwezi mmoja kila siku mpaka iwe ni tabia.

Acha kuvuta sigara, kunywa kahawa na soda kwa wingi, kula lishe nzuri ili kuepusha meno kuchafuka. Jiwekee tabia ya kunywa zaidi maji baada ya kula ama kunywa juisi yoyote, kusaidia kuepusha madhara ya kitu hicho kwenye meno.

2.Coconut oil pulling

Coconut oil pulling ni mja ya njia murua kabisa ya kusafisha bakteria wabaya mdomoni mwako na kukuacha na harufu nzuri ya kinywa sikuzote na meno meupe. Ni njia salama na ya asili isiyohitaji matumizi ya kemikali mbaya wala dawa ambazo zina madhara makubwa.

Nimekuwa nikishauri mamia ya watu na wamefanikiwa kuondoa adha hii ya kunuka mdomo na meno machafu kupitia coconut oili pulling. Wewe pia unaweza kuwa mmoja wa mashuhuda wetu kama tu utazingatia kwa makini step za kufuata.

Coconut oil pulling kama jina lake lilivyo ni kitendo cha kuvuta uchafu na bacteria ka vile sabuni inavyonyonya uchafu kwenye nguo wakati wa kufua nguo. Lakini kwenye upande wa kinywa unanyonya bacteria na uchafu kwenye meno kwa kutumia mafuta ya kupikia ya nazi.

Hatua za kusafisha meno kwa mafuta ya nazi

  1. Hakikisha unafanya oil pulling asubuhi unapoamka kabla ya kula na kunywa kitu chochote
  2. Chukua kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya kupikia ya nazi kisha weka mdomoni, anza kuzungusha ulimi na kuyasambaza mdomo wote taratibu kwa dakika 10 mpaka 20
  3. Baada ya muda huu tema uchafu wote bila kumeza hata kidogo kisha safisha mdomo na maji, unaweza kutumia maji yenye chumvi ili kuondoa mafuta yote.
  4. Hakikisha usiteme kwenye sink tema nje ili kuzuia kuziba kwa mafuta kwenye sinki
  5. Brush meno yako kama kawaida
  6. Rudia kitendo hiki mara 3 mpaka 5 kwa week kupata matokeo mazuri

3.Apple cider vinegar

Pamoja na faida zake kwenye mapishi na kupunguza uzito, apple cider vinegar ni nzuri sana katika kutoa uchafu sugu uliogandamana kwenye meno yako. Apple vinegar inafaa sana kwa uchafu uliosababishwa na kahawa na sumu ya nicotine kwa uvutaji sigara.

Nini siri iliyopo kwenye apple cider vinegar?

ina viambata hai vya acetic acid, potasium, magnesium na viambata cvya kuchakata chakula (enzymes)ambazo zinaua bakteria wabaya pia hapohapo inachochea ukuaji wa bakteria wazuri kwenye mfumo wa chakula.

Hakikisha unatumia apple vinegar kw amuda mrefu kupata matokeo. Siyo njia ya kukuletea matokeo haraka, jipe walau mwezi mmoja kwa meno yako kuanza kun’gaa.

Matumizi: Chovya kiasi kidogo cha apple vinegar kwa kidole, kisha pakaa kwneye meno yako una usugue kwa dakika moja taratibu. Baada ya hapo brush meno yako kawaida kwa dawa uuliyozea kuitumia.

Angalizo; Vinegar ina utindikali hivo sugua meno taratibu sana unapotumia vinegar.

4.Tumia maganda ya limau au chungwa

Kama ilivyo kwa apple cider vinegar, maganda ya matunda haya yana kemikali ambazo husaisidia kuondoa uchafu kwene meno na kukuacha na tabasabu zuri. Matumizi: chukua ganda la limau au chungwa, sugua meno yako machafu kwa dakika moja, kisha osha kwa maji na upige mswaki kikawaida.

5.Mkaa

Mkaa husaidia kunasa vimelea wabaya na kufyonza sumu kwenye meno yako. Kufanya meno kuwa meupe kwa kutumia mkaa, chonya mswaki wako kwenye maji kisha pakaa unga kidogo wa mkaa na ubrush meno yako. Safisha zaidi kwenye meno machafu.

Baada ya hapo utasafisha meno yako kwa dawa ya meno. fanya zoezi hili mara tatu tu kwa wiki, sitisha zoezi kama utaisikia vibaya au kama una pumu.

Hatari ya kutumia njia za kisasa kusafisha meno

Tafiti zinaonesha kwamba kusafisha eno kupitia njia za kisasa zinaharibu na kufanya meno kuwa dhaifu. Dawa nyingi za kusafisha meno zinazouzwa famasi zina kemikali mbaya za carbamide peroxide. Kemikali hii huzalisha urea ambayo hupelekea meno kuoza na kubomoka. Kemikali hizi pia hufanya meno kuwa dhaifu na kushindwa kun’gata vitu vigumu.

Tumia njia hizi endapo tu njia asili nilizoeleza pale juu hazijakupa matokeo katika kipindi cha mwezi mmoja. Kumbuka tu kwamba njia nzuri ya kusafisha meno na kinywa chako ni kwa kula lishe bora. Kusafisha meno vizuri kila siku asubuhi na jioni, kuepuka vyakula hatarishi kama vya sukari na kuacha sigara.

Categories
Urembo wa ngozi

Njia Asili za Kuondoa Michirizi kwenye ngozi

kuondoa michirizi kwenye ngozi
michirizi kwenye ngozi

Wanawake wengi kwa sasa wanatafuta njia gani salama za kuondoa michirizi kwenye ngozi. Michirizi na mikunjokunjo kwenye ngozi ya mapaja, tumbo na kwenye mikono ni tatizo linalowatesa zaidi wanawake. Kwani wengi wanahangaika ili kuondokana na tatizo hili bila mafanikio. Pamoja na kutumia vipodozi na cream mbalimbali bado tatizo halijaisha.

Tatizo linapelekea wadada kuona aibu, kushindwa kujiachia na kutovaa nguo wanazozitaka kwa kuogopa mikunjokunjo kuonekana.  Makala yangu ya leo itaangalia tatizo kwa upana wake na kukupa mpangilio wa lishe na ushauri wa kina. Pamoja na njia za asili za kutibu tatizo lako ili ufurahie urembo wako wa mwili, karibu.

Michirizi au cellulite ni kitu gani?

Cellulite ni mwonekano wa mikunjokunjo na mistari kwenye ngozi ya mwili. Mistari hii hutokea zaidi kwenye eneo la tumbo, chini ya mikono, kwenye mapaja na matako. Michirizi hutokea zaidi kadiri umri unavoenda. Baadhi ya vitu vinavyoletekeza mikunjokunjo kwenye ngozi ni pamoja na kuvurugika kwa homoni, pamoja na kutokufanya mazoezi.

Wanawake wanapata zaidi Michirizi kuliko Wanaume

Tatizo hili huwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume ambapo kutokana na unene. Unene kupita kiasi hupelekea leya ya ndani yenye mafuta (fat globules) kuwa na msuguano na tishu za ngozi na hivo kupelekea mikunjokunjo na michirizi kwenye ngozi.

Tafiti zinasema kwamba asilimia 80 ya wanawake wana tatizo hili la cellulite. Ambapo wengi wanalipata kadiri wanavozeeka kwa ngozi kupungua uwezo wa kuvutika na kusababisha nyama kuanguka na kuleta mikunjokunjo.

Kuwa na michirizi siyo tatizo kubwa kiafya ndio maana wengi huliacha kama lilivyo bila kushughulika nalo. Lakini kama wewe ni mwanamke unayependa urembo na unapenda kujiachia maeneo kama beach na sehemu za wazi basi hiki kitakuwa kikwazo sana. Maana utaogopa kuonekana na watu kwamba ngozi yako ina kasoro ndio maana nimeandika makala hii ikusaidie.

Nini kinasababisha Michirizi Kwenye Ngozi

Mazingira hatarishi na sababu zinazochangia upate mikunjokunjo na michirizi kwenye ngozi ni pamoja na

  • lishe mbovu
  • mwili kubakiza maji tumboni (fluid retention ambapo wakati mwingie hupelekea tumbo kujaa gesi)
  • damu kutozunguka vizuri
  • udhaifu wa tishu zenye collagen na kuepelekea kujikunja kiurahisi
  • mabadiliko ya homoni
  • mwili kukosa mazoezi na kutoshugulika
  • msongo wa mawazo kupita kiasi ambao hupunguza uzalishaji wa collagen: collagen ni kiungo kilichosheni protini ambacho kinatengeneza shape na tishu za ngozi, hivo kufanya ngozi ya mtu kuonekana bado changa.
  • historia ya magonjwa mfano magonjwa ya autoimmune, kisukari, watu wanaovuta sigara na wenye alegi/mzio.

Sasa umejifunza jinsi sababu za kimaisha zinavoharibu mwonekano wa ngozi yako na tayari umejua chanzo cha tatizo lako kuwa ni kwenye lishe. Ni wazi sasa kwamba dawa na cream za kupata kwenye ngozi au mikanda ya kuvaa ili upunguze michirizi siyo suluhisho salama na la kudumu. Bali unatakiwa kubadili mtindo wa maisha  kwenye lishe na kuweka ratiba ya mazoezi.

Tiba Asili ili Kuondoa Michirizi na Mikunjokunjo kwenye Ngozi Yako

Hizi ni njia zangu 5 zitakazokusaidia kuondoa shida ya michirizi.
Angalizo: Kama wewe unataka njia za haraka haraka basi hutazipata hapa. Maana ninaelekeza namna ya kubadili mtindo wa maisha ili uepuke tatizo miaka yote, na itachukua muda kupata matokeo.

1.Kula Lishe Bora

Kama tulivosoma pale juu kuna uhusiano mkubwa kati ya uzito mkubwa na kitambi na kupata mikunjokunjo. Hivo punguza vyakula vya wanga na sukari na kula zaidi vyakula vya mafuta kama nyama, parachichi, nazi na mafuta ya nazi, samaki nk. Weka ratiba ya kupunguza unene wako uliopitiliza kwa kufanya mazoezi na kushugulisha mwili wako.

2.Tumia Collagen ya Kutosha

Kama tulivojifunza mwanzoni ni kwamba tishu za ngozi zimetengenezwa kwa protini za collagen. Kwahiyo kama ngozi yako ipo imara basi utapunguza uwezekano wakupata mikunjokunjo. Collagen ni protini inayopatikana kwa wingi kwenye ngozi na husaidia kuvutika na kufanya ngozi kuwa hai na laini.

Chanzo kizuri cha Collagen ni kunywa supu ya mifupa (bone broth) . Supu ya mifupa ina amino acid kwa wingi ambazo hutengeneza collagen. Collagen iliyopo kwenye Supu ya mifupa  husaidia kuimarisha tishu za ngozi na kuondoa tatizo la cellulite.

3.Tumia virutubisho

Virutubisho vya kuondoa mikunjokunjo kwenye ngozi na michirizi (anti-cellulite suppliments): Unaweza kufika ofsini kwetu ukatumia virutubisho kama royal gel na sipiriluna vikakusaidia kupambana na tatizo lako bila kikwazo.

4.Fanya mazoezi kila mara

Mazoezi ni njia nzuri sana pale unapotaka kupunguza uzito. Tumeona pale juu athari za uzito mkubwa na kitambi kwenye kupata mikunjokunjo, pamoja na kula lishe nzuri ni muhimu sasa uweke ratiba ya kufanya mazoezi walau mara tatu kwa week.

5.Tumia mafuta asili ya nazi kwenye kutibu ngozi yako.

Unaweza kutumia mafuta halisi ya nazi kwa kupaka kwenye ngozi yako baada ya kuoga. Kumbuka cream za madukani zinaweza kuwa ghali na hatari kwa afya yako kwa maana zina kemikali na metali nzito ambazo ni sumu kwa afya ya ngozi.

Maelezo ya Mwisho pale Unapopambana na michirizi+mikunjokunjo

  • Cellulite ni mwonekano wa mikunjokunjo kwenye ngozi na hii ni kutokana na kusuguana kwa tabaka la mafuta na tishu za ngozi
  • Sababu zinazopelekea upate mikunjokunjo kwenye ngozi ni pamoja na uzito mkubwa, lishe mbaya, kubakiza maji ama mwili kukosa kabisa maji, matatizo kwenye usafirishaji mwilini na udhaifu wa tishu zenye collagen kwenye ngozi
  • Kupunguza uzito, kula vyakula asili vyenye kambakamba na kufanya mazoezi ,  husaidia kupunguza sana tatizo la cellulite.

Mafuta ya lavender yanasaidia kuondoa michirizi

lavender oil

Mafuta ya lavender au mrujuani ni moja ya mafuta yanayotumika zaidi kwenye kundi la (essential oil) lakini faida zake ziligunduliwa kwa zaidi ya miaka 2500 iliyopita katika kutibu magonjwa na matatizo ya ngozi.

Matumizi ya mafuta ya lavenda kwa kupakaa kwenye ngozi huzuia na kuondoa chunusi na matatizo mengine ya ngozi kama madoa, michirizi, mikunjokunjo na pia kupunguza kasi ya kuzeeka kwa ngozi.

Mafuta ya levender yamekuwa adimu sana kutokana na uwezo wake mkubwa kupambana na matatizo ya ngozi. Fika ofsini hapa Magomeni Mwembechai upate mafuta haya ambayo ni original na asili. Gharama ya mafuta ni sh 40,000/=

Tuandikie whatsapp kwa namba 0678626254 kupata tiba ya tatizo lako

Soma makala inayofuata kuhusu: Kubana tumbo baada ya kujifungua

Categories
Natural remedies

Faida 8 za kunywa Green Tea

green tea
green tea

Green tea inasemekana kwamba ni moja ya kinywaji chenye afya sana duniani, na kinachopendwa zaidi.

Chai hii imejaa viondoa sumu vingi sana ambavyo vitakusaidia kuimarisha afya ya ubongo, kupunguza mafuta mabaya mwilini, kukulinga dhidi ya saratani na kupunguza hatari ya kuugua magonjwa ya moyo. Hapa chini ni maelezo ya nane za kunywa green tea.

1.Green tea ina viambata hai muhimu kwa ajili ya afya yako

Green tea ni zaidi tu ya chai kama ulivozoea. Ina viambata vya polyphenols, ambavyo vitakusaidia kupunguza mpambano(inflammation) kwenye mwili na pia kupambana na saratani.

Pia green tea ina viambata vya epigallocatechin-3-gallate(EDCCG). Viamabata hai hivi husaidia kuzuia madhara ya sumu mwilini na kulinda seli za mwili dhidi ya sumu.

2.Kuimarisha afya ya ubongo

Green tea inafanya kazi nzuri katika kukuweka kuwa mchangamfu na kuimarisha uwezo wa ubongo. Kiambata kikubwa ambacho kinaboost ubongo ni caffeine.

Usiogope kwamba ina caffeine nyingi kama kahawa hapana. Green ina kiwango kidogo tu cha caffeine ambacho kitachochea uzaishaji wa kemikali za dopamine na norepinephrine ambazo hufanya ubongo wako upige kazi zaidi.

Pia green tea inachochea ufanyaji kazi wa kemikali ya GABA. GABA ni ant-anxiety yaani inazuia msongo wa mawazo na hivo kukufanya ujisikie vizuri.

3.Kuondoa mafuta mabaya mwilini

Licha ya kuwa kiburudisho kizuri, green tea inachochea uwezo wa mwili kuunguza mafuta mabaya na hivo kupunguza uzito na nyama uzembe. Green tea inachochea shughuli za mwili na kupelekea mafuta kuunguzwa kuwa nishati.

4.Kupunguza hatari ya kuugua baadhi ya aina za saratani

Saratani husababishwa kukua kupita kiasi kwa seli za mwili. Ni moja ya ugonjwa unaaongoza kwa kusababisha vifo vingi sana duniani.

Tafiti zinasema kwamba seli zinapoathiriwa na sumu hupelekea seli hizi kuvimba na kuanzia kukua kupita kiasi. Viambata amana antioxidants zilizopo kwenye green tea husaidia kuzuia madhara ya sumu ambazo hupelekea saratani.

Tafiti zimebaini kwamba viondoa sumu vya kwenye green tea husaidia kupunguza hatari ya kupata aina hizi za saratani

Ili upate faida zaidi za green tea, epuka kuchanganya na maziwa. Baadhi ya tafiti zinasema kwamba unapochanganya na maziwa inapunguza ufyonzaji wa viondoa sumu.

5.Kulinda ubongo dhidi ya magonjwa ya uzee

Pamoja na kuimarisha ufanyaji kazi wa ubongo, green tea inasaidia kupunguza ubongo kuzeeka. Magonjwa makubwa yanayowakumba wazee kutokana na ubongo kuzeeka ni pamoja na Alzheimer na Parkinson. Magonjwa haya hupelekea ubongo kupungua uwezo wa kumbukumbu na pia kupunguza uwezo wa kufikiri.

6.Green tea itakusaidia kutibu harufu mbaya mdomoni.

Streptococcus mutans ni bakteria wanaopatikana sana kwenye mdomo. Bakteria hawa husababisha uchafu kuganda kinywani na kupelekea harufu mbaya na meno kuoza.

Kiamabata hai cha catechins kilichopo kwenye green tea kinasadia kudhibiti ukuaji wa bakteria hawa na hivo upunguza athari yake kwenye kinywa ikiwemo kuondoa harufu mbaya.

7.Green tea yaweza kukukinga na Kisukari cha Ukubwani.

Kisukari cha ukubwani ama type 2 diabetes ni aina ya kisukari inayompata mtu kuanzia miaka 20 kwenda juu. Aina hii husababishwa na mwili kushindwa kutumia insulini inayomwagwa kwenye damu ili kushusha sukari. Au mwili kutozalisha kiwango kinachotakiwa cha insulini.

Tafiti zinasema kwamba green tea husaidia kuongeza mwitikio wa mwili kwenye insulini na hivo kuzuia sukari kupanda kupita kiasi kwenye damu.

8.Green tea yaweza kuzuia magonjwa ya moyo

Magonjwa ya mfumo wa damu ikiwemo ikiwemo magonjwa ya moyo na stroke, ni moja ya chanzo kikubwa acha vifo duniani kote.

Tafiti zinasema kwmaba green tea yanweza kupunguza hatari ya kuugua magonjwa haya, kwa kupunguza mafuta mabaya mwili (bad cholesterol).

Green tea pia inaongeza viondoa sumu kwenye damu, na hivo kulinda mishipa ya damu dhidi ya athari ya mafuta mabaya(LDL). Mafuta haya mabaya huweza kusababisha damu kuganda na hivo kuzuia usambazaji wa hew aya oxygen mwilini.

Unahitaji Green kutibu changamoto zako? Agiza kutoka kwetu green tea zenye ubora mkubwa kwa Tsh 50,000/=

Hapa chini ni picha na maelezo mafupi kwa kila green tea zetu. Kumbuka hizi ni zaidi ya chai, ni tiba kwa magonjwa yako ya kiafya. Chagua unayohitaji kisha fika ofsini kuchukua. Ikiwa upo mkoani tutakutumia. Kila chai tiba ni tsh 50,000/=

Unahitaji maoni na Ushauri? Tuandikie kwa Whatsapp namba 0678626254. Usipige simu namba ni ya whatsapp tu

Bofya kusoma makala inayofuata: Chanzo cha fangasi mdomoni+tiba