Categories
Magonjwa ya Kuambukiza

Tetekuwanga

tetekuwanga
tetekuwanga

Nini maana ya Tetekuwanga?

Tetekuwanga ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza. Ugonjwa unasababishwa na kirusi anayeitwa varicella-zoster. Watu wengi wanaugua tetekuwanga wakiwa wadogo, endapo hawakupata chanjo.

Mtoto anayeugua tetekuwanga anaweza kumwambukiza mtoto mwingine kwa urahisi sana. Kwa sasa tatizo siyo kubwa ukilinganisha na zamani kwani watoto sasa wanaweza kuachanjwa ili wasipate tetekuwanga.

Huwezi kuugua tetekuwanga mara mbili

Ukishaugua tetekuwanga huwezi tena kuugua maisha yako yote hata kama ukigusana na mgonjwa. Kama hujachanja unaweza kuugua tetekuwanga katika umri wowote ule.

Watu wazima wanaougua tetekuwanga wanakua wadhaifu sana na ugonjwa ukawapelekesha mno ukilinganisha na watoto. Ni bora kuugua tetekuwanga ukiwa mtoto kuliko kuugua ukubwani, au upate chanjo kabisa ili uisugue.

Tetekuwanga inaambukizwaje?

Unaweza kupata tetekuwanga kwa

 • kugusana na mgonwa mwenye tatizo
 • kuvuta hewa ya mgonjwa watetekuwanga au majimaji ya kooni na mafua
 • kugusa majimaji ya mgonjwa kwenye pua zako, mdomo na macho

Je kuna uhusiano gani kati ya tetekuwanga na mkanda wa jeshi?

Ukishaugua tetekuwanga, wale virusi wanabaki mwilini lakini hawasababishi tena tetekuwanga. Lakini siku virusi hawa wakiibuka wataleta ugonjwa mwingine unaoitwa mkanda wa jeshi ama shingles. Kwahivo mkanda wa jeshi hauambukizwi bali ni virusi wako wa tetekuwanga ulougua zamani ndo wanakuletea ugonjwa mpya.

Kumbuka watu wenye mkanda wa jeshi hawawezi kumuambukiza mtu mkdanda wa jeshi, basi wanaweza kumpa tetekuwanga, endapo huyo mtu hakuwahi kuugua tetekuwanga. Mkanda wa jeshi nao huisha wenyewe ndani ya week .

Dalili za tetekuwanga

Dalili za tetekuwanga hazijifichagi, ni rahisi sana kumtambua mgonjwa wa tetekuwanga. Dalili hizi ni kama

 • Homa
 • Kuhisi uchovu
 • kichwa kuuma
 • Maumivu ya tumbo
 • Malengelenge kwenye ngozi yanayowasha na kutoa maji
 • Makovu baada ya lengelenge kutoboka
 • Ngozi yenye madoadoa

Vipimo kugundua uwepo wa tetekuwanga

Kwa kutumia tu macho, muhudumu wa afya anaweza kugundua kwamba unaumwa tetekuwanga.

matibabu na huduma kwa mgonjwa wa tetekuwanga

Nawezaje kumsaidia mwanangu anayeumwa tetekuwanga?
Hakikisha mtoto anapata mda mwingi wa kupumzika na kunywa maji ya kutosha. tetekuwanga huwa inapona yenyewe ndani ya week 1 au mbili. Kumsaidia mtoto na muwasho unaweza kufanya haya

 • weka nguo yenye majimaji baridi kwenye lengelenge
 • hakikisha mwanao yupo eneo lenye ubaridi
 • ongea na mwanao asitoboea lengelenge kama mtoto mdogo sana mkate kucha ili ajijikune
 • unaweza kumpaka lotion maalumu au ukampa dawa zenye kiamabata cha antihistimine- nunua pharmacy
 • mwogeshe mwanao kwa maji baridi mara kwa mara. Mfute mtoto kwa taulo kama unakanda mwili, usifute kwa kusugua.

Usimpe mtoto dawa za asprin. Hizi zinaweza kumletea mtoto shida hasa mwenye homa. Kama huna uhakika dawa ipi ya kumpa mwanao, nenda pharmacy jieleze utapewa dawa sahihi.

Je kuna madhara zaidi yanaweza kutokea kwa mtoto mwenye tetekuwanga?

Changamoto kubwa zinazoweza kujitokeza kutokana na tetekuwanga ni pamoja na

 • bakteria kushambulia ngozi, damu na tishu laini
 • Nimonia- yani mapafu kujaa maji
 • mwili kupungukiwa maji kupita kiasi
 • ini kuathirika
 • damu kuganda

Nani anaweza kuugua zaidi na kulemewa na tetekuwanga?

Watu wenye afya njema, wanapougua tetekuwanga, huwa haiwapelekeshi sana. Japo wa watoto wadogo sana kuugua tetekuwanga inaweza kuwaletea shida zaidi, pia wenye mimba, wenye kinga dhaifu . Wagonjwa wa Ukimwi, saratani na wanapata tiba ya mionzi wanalemewa sana na tetekuwanga

Je tetekuwanga yaweza kuua mtu?

Ni mara chache sana tetekuwanga ikahatarisha maisha ya mtu. Watu wengi hupona mapema ndani ya wiki mbili baada ya kuugua. Japo wapo watu waliowahi kufa kwasababu ya tetekuwanga.

Je mwanangu anaweza kupata chanjo ya tetekuwanga?

Jibu ni ndio kuna chanjo ya tetekuwanga, ongea na mtoa huduma hospital atakupa maelekezo.

Je watu wazima wanaweza kuugua tetekuwanga?

Mtoto akishaugua tetekuwanga, mwili wake unapambana na virusi hao na kutengeneza kinga ya kudumu. Kinga hii inakaa mwilini miaka yote ya uhai wako, na itapambana na virusi wageni wataakaoingia siku zijazo.

Ni lini unatakiwa kumwona daktari?

Nenda hospital haraka endapo mtoto wako anapata dalili za

 • ana malengelenge kwe nye macho
 • kuumwa sana kichwa
  • ana malengelenge makubwa yanayotoa usaha
  • anashindwa kupumua vizuri

  Bofya kusoma kuhusu: kwanini unaugua kaswende sugu

  Categories
  Afya ya mwanamke na uzazi

  Dalili Mbaya Kwa Mjamzito

  dalili mbaya kwa mjamzito
  mjamzito

  Kipindi cha ujauzito kinaambatana na mabadiliko mengi sana ya mwili, pamoja na mabadiliko ya kimaisha pia kwenye kujiandaa kumpokea mwanafamilia mpya. Ni kipindi pia ambacho waweza kuwa na hofu sana kuhusu mimba yako, na utakuwa mwangalifu sana. Hapa chini ni maelezo a kina juu ya dalili mbaya kwa mjamzito na hatua za kuchukua mapema.

  Mabadiliko mengi ambayo utayaona mwilini mwako, jua kwamba ni kawaida na ni lazima uyapitie. Dalili nyingi mfano kuumwa nyonga, tumbo kuunguruma, kukosa choo, kizunguzungu nk zinakuja na kupotea.

  Je dalili mbaya zinaisha mapema?

  Baadhi ya dalili waweza kukaa nazo mpaka siku unajifungua, na kuna zingine zinakuja na kupotea. Hapo ndipo yatakiwa kuwa makini kwa kila dalili unazopata. Kuna dalili zingine hatari ambazo haitakiwi upitishe hata siku 1 bila kwenda hospital, endapo utaziona.

  Dalili za Kawaida Ambazo siyo hatarishi

  Dalili nyingi kati ya hizi siyo hatari, na haitakiwi kupata hofu sana. Japo unaruhusiwa kumpigia daktari wako na kumuuliza ili upate uhakika zaidi. Dalili nyingi ya hizi zinajitokeza mimba ikiwa changa, na zingine baadae

  • kutapika
  • kutokwa na uchafu mwingi ukeni
  • kichwa kuuma
  • uchofu na kizunguzungu
  • maumivu yanayokuja kwa haraka na kupotea
  • kupungua uzito
  • kuhisi joto kali
  • kushindwa kuvuta hewa vizuri
  • mawazo, na kupata hofu ana kushindwa kufanya kazi zako vizuri

  Dalili mbaya kwa mjamzito.

  Dalili hizi zinatokea mda wowote wa ujauzito. Japo mimba inapokuwa changa zaidi ndipo hatari ya mimba kuharibika inakuwa kubwa, ila watakiwa kuwa makini kipindi chote.

  Dalili hatarishi ni pamoja na

  1.Kuvuja damu

  Kitendo cha kutokwa damu/bleed ukiwa na mimba siyo ishara nzuri hata kidogo, ni kiashiria kwamba kuna tatizo. ikiwa unatokwa damu nzito, na una maumivu makali ya tumbo upande wa kushoto au kulia na unajihisi kuishiwa nguvu, hii inaweza kuashiria mimba imetunga nje ya kizazi.

  Mimba ikitunga nje ya kiazi haiwezi kukua, inatakiwa kuondolewa ma[pema kwa upasuaji. Mimba hiozi huitwa ecopic, endapo haitaondolewa mapema, mgonjwa anaweza kupoteza maisha.

  Kama damu zinatoka nzito, tumbo linauma kuzunguka kitovu, hii inaashiria mimba imeharbika, na hii inatokea zaidi mimba ikiwa chini ya wiki 12. Sisemi kwamba mimba kubwa kubwa haziharbiki, hapana. Ni kwamba mimba nyingi zinaharbika zikiwa changa.

  2.Kutapika na kichefuchefu kupita kiasi

  Kwa mjamzito ni kawaida kupata kichefuchefu, lakini kama tatizo ni kubwa inaweza kuashiria shida kubwa ya kiafya. Kama unashindwa mpaka kula au kunywa chochote, hapo utaishiwa maji. Na kuishiwa maji inaweza kuhatarisha ujauzito wako.

  Kama unahisi kizunguzungu kinakutesa sana, ongea na daktari atakupa dawa ya kupunguza makali yake.

  3.Mtoto kuacha kucheza

  Mtoto kupunguza kucheza inaweza kuashiria kachoka, hii ni kawaida isikupe hofu. ila kama hachezi kabisa kwa siku nzima, hapo kuna shida kubwa.

  Sasa ili kugundua tatizo, inashauriwa ukiona mtoto hachezi mda mefu, jaribu unywe kitu cha baridi. Kisha lala kwa ubavu, na fatilia kama mtoto ataanza kucheza.

  Mpigie daktari, ama nenda hospital haraka endapo utagundua mtoto ameacha kucheza. Daktari atafanya vipimo kuona kama kuna hatari yoyote.

  4.Kupata uchungu mapema mimba ya miezi 7

  Kupata uchungu na mimba haijatimiza umri wa kujifungua, ni dalili mbaya. Kama tumbo linavuta na kuachia na hii hali itokee mara chache na kuisha hilo ni kawaida. Kwani hata ukifika kileleni baada ya tendo, lazima utahisi tumbo kuvuta.

  Lakini endapo tumbo linavuta na kuachia, kisha baada ya dakika 10 linaanza tena kuvuta na kuachia, hiyo ni ishara ya kuelekea kuzaa njiti. Mpigie daktari mapema endapo utaona hali hii.

  5.Chupa kupasuka mapema ni dalili mbaya kwa mjamzito

  Tunaposema chupa, tunamaanisha ule mfuko unaobeba mtoto. Mfuko huu unakuwa na maji yanayomlinda mtoto asiumie. Mfuko unapasuka pale mama akianza uchungu na yupo tayari kujifungua. Endapo mfuko utapasuka mapema na mtoto akaendelea kubaki tumboni, mtoto atakosa hewa na kupoteza uhai.

  Maji haya ni tofauti na mkojo, kwani hayaishi mapema yakianza kuvuja. Kwahivo tazama ukiona dalili ya kuvuja maji ukeni, tena maji mengi, nenda hospitali haraka.

  6.Maumivu makali yasiyoisha kwenye kichwa, tumbo na kushindwa kuona vizuri

  Hizi dalili zinaweza kuashiri kupanda kwa presha kitaalamu (preeclampsia) . Hili ni tatizo baya na linaweza kupelekea kifafa cha mimba. Tatizo linaambatana na dalili za presha kupanda na protini nyingi kwenye mkojo, hasa inatokea baada ya week 20 za ujauzito. Hakikisha unaenda hospital haraka endapo unahisi dalili hizo.

  Nawezaje kujizuia nisipate dalili mbaya kwa ujauzito wangu?

  Ukweli ni kwamba ni vigumu sana kujizuia asilimia zote kupata dalili mbaya kwenye ujauzito. Lakini kuna vitu vichache unaweza kufanya kupunguza hatari ya mimba kuharibika kabla ya muda wake.

  Hudhuria clinic zote na upate dawa za kuongeza damu mapema kabisa. Unapoenda clinic daktari atachukua historia yako na kukwambia endapo upo kwenye kundi hatarishi. Utapewa ushauri wa kina kuhusu lishe na afya ya akili pamoja na afya ya tendo la ndoa.

  Bofya kusoma kuhusu kifafa cha mimba

  Categories
  Nguvu za Kiume Tendo la ndoa

  Viagra,Matumizi, Faida na Madhara

  viagra
  viagra

  Naamini umekuwa ukisikia hili neno kwa muda mrefu sana, pasipo kujua undani wa dawa hii ya viagra. Leo nitakweleza kwa undani kuhusu viagra, ikiwemo matumizi, upatikanaji, madhara yake ya mda mrefu na kitu gani waweza kutumia kama mbadala wa viagra.

  Viagra ni kutu gani?

  Endapo unawahi kufika kileleni ama unashindwa kusimamisha uume vizuri wakati wa tendo la ndoa. Ukienda hospitali, daktari anaweza kukuandikia utumie viagra. Hii ni dawa daktari anakwandikia kusaidia nguvu za kiume.

  Viagra inakuja katika mfumo wa vidonge na hutakiwi kutumia mpaka uandikiwe na daktari, na utatumia kabla ya tendo siyo kila siku.

  Viagra inafanyaje kazi?

  Uume unasimama pale protini inayoitwa cyclic guanosine monophosphate(cGMP) inapotolewa kwenye damu, na kupelekea mzunguko mkubwa wa damu kuelekea kwenye uume. Mzunguko wa damu ukiwa mkubwa kuelekea kwenye uume hapo utaweza kudindisha vizuri na kupiga show mda mrefu bila kuchoka.

  Je inachukua mda gani kwa Viagra kufanya kazi?

  Viagra inaleta matokeo haraka sana baada tu ya kumeza dozi yako. Viagra inafanya kazi ndani ya lisaa. Kwa watu wachache inaweza kuanza kazi ndani ya nusu saa tu baada ya kumeza, na wengine mpaka baada ya masaa ma4.

  Je vipi kama Viagra haitafanya kazi?

  Endapo viagra haitafanya kazi, hakikisha unamjulisha daktari aliyekuhudumia. Daktari anaweza kupendekeza utumie dozi kubwa zaidi ya dawa, kisha ataendelea kukufatilia kama dozi hiyo kubwa imefanya kazi.

  Je Nguvu a Viagra inaisha Ndani Ya Muda Gani?

  Viagra inafanya kazi vizuri ndani ya masaa kadhaa baada ya kumeza. Kwa watu wengi dawa inafanya kazi ndani ya lisaa tu na kwa tu wachache dawa itaendelea kukupa nguvu mpaka masaa ma4. Kadiri mda unavosogea nguvu ya viagra inapungua na baadae kuisha. Hapo utahitaji kumeza tena ikiwa unataka kushiriki.

  Kwahivo ieleweke hii siyo tiba ya tatizo lako. Ni booster tu ya mda mfupi ili ufurahie tendo, kisha utarudi kule kule.

  Je Vigra inatumika Kwa Wanawake?

  Pengine unajiuliza je mwanamke naye anatumia kuimarisha nguvu za kike? Dawa hii imethibitishwa kutumika kwa wanaume tu kwenye tatizo la uume kutosimama imara.

  Je Kuna Matokeo/madhara Gani Kutumia Viagra?

  Kama ilivo kwa dawa zingine zote, Viagra yaweza kuwa na madhara madogo na hata makubwa pia. Hapa chini ni list ya madhara yanayoweza kujitokeza. Kumbuka madhara haya yanatofautiana na umri wa mtu. Magonjwa mengine aliyonayo na pia dawa anazotumia kwa sasa.

  Dalili/matokeo Ya Mda Mfupi

  Dalili mbaya au matokeo yanaweza kujitokeza baada ya kumeza viagra ni pamoja na

  • kichwa kuuma
  • makamasi kwenye koo
  • maumivu chini ya mgongo na misuli
  • kizunguzungu
  • kiungulia na
  • mabadiliko kweneye kuona

  Madhara Makubwa ya Viagra

  Madhara makubwa yanaweza kujitokeza ukimeza viagra, ila usiogope, hayajitokezi mara kwa mara. ikiwa umepata matokeo haya, mweleze daktari mapema. Matokeo haya ni pamoja na

  • kushindwa kuona
  • kupata aleji
  • presha kushuka sana
  • kupata shambulizi la moyo
  • kupungua uwezo wa kusikia na pia
  • kuumia sana wakati wa kukojoa mbegu
  • uume kukosa nguvu kabisa kwenye tendo hasa ukitumia viagra kwa mda mrefu

  Jinsi ya Kutumia Viagra

  Kwasababu dawa unaandikiwa hospitali, ni lazima daktari, ni lazima akwandikie matumizi ya dawa. Muhimu sana kufatilia maelekezo uliopewa na daktari wako. Viagra zinapatikana wa nguvu za ujazo tofauti, yani mg 25, mg 50 na mg 100.

  Muda gani unatakiwa kumeza viagra

  Viagra inatakiwa kumezwa pale tu inapohitajika, yani lisaa limoja kabla ya kwenda kufanya ngono. Haitakiwi kumezwa mara kwa mara. Hutakiwi kabisa kumeza viagra zaidi ya mara moja kwa siku.

  Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu viagra

  1.Je viagra inaongeza hamu ya tendo la ndoa?

  Jibu ni hapana, viagra haiongezi hamu ya tendo. Unatakuwa uwe na msisimko tayari wa kuifanya tendo ili viagra ifanye kazi . Kazi ya viagra ni kuongeza msukumo wa damu kuelekea kwenye uume ili usimame vizuri kwenye tendo.

  2.Je viagra inazuia kumwaga mbegu? au kukufanya umwage mbegu mara nyingi zaidi?

  inawezekana kabisa viagra kubadili mfumo wa utoaji mbegu kama ilivokuwa mwanzo/ mabadiliko haya ni pamoja na

  • kukuzuia kumwaga mbegu
  • kufanya umwage mbegu mara nyingi zaidi

  Kama unapata changamoto baada ya kutumia viagra, ongea na daktari aliyekuhudumia.

  3.Je Viagra inafanya uume uendelee kusimama hata baada ya kumwaga mbegu?

  Ndio, viagra yaweza kukufanya uendelee kusimamisha hata baada ya kumwaga mbegu. Lakini endapo uume utasimama zaidi ya masaa ma4 muone daktari haraka. Hii inaweza kuwa hali ya hatari inayohitaji usaidizi wa haraka, maana itaharibu uume wako.

  4.Je Viagra inaongeza ukubwa wa uume wako?

  Hapana, ni ngumu sana viagra kuongeza ukubwa wa uume wako kuliko kawaida. Uume utavimba tu wakati una hisia za tendo, ukimaliza tendo uume unarudi kawaida. Viagra itafanya tu uume usimame na uwe imara kuliko kawaida ila siyo kuongeza maumbile.

  Makundi ya watu wasiotakiwa kutumia Viagra

  Viagra yaweza isikufae endapo una matatizo baadhi ya kiafya. Ongea na daktari vizuri na mweleze historia yako yote kabla hujaanza kumeza viagra. Magonjwa ama changamoto hizo ni pamoja na

  • magonjwaya moyo, stroke ama umefanyiwa upasuaji wa moyo ndani ya miezi 6
  • uume wako una maumbile yasiyo kawaida , mfano umejikunja sana, ama unapata mjeraha mara kwa mara.
  • Magonjwa ya damu kama sickle cell
  • magonjwa ya moyo
  • una presha ya kushuka
  • una changamoto za kutokwa damu mfano puani na kwingine kwenye matundu
  • vidonda vya tumbo: Hakikisha unamweleza daktari ikiwa unaumwa vidonda tumbo
  • magonjwa ya figo na ini: kama figo na ini zina hitilafu, kumeza dawa yaweza kuongeza sumu mwilini na kuleta shida zaidi.

  Viagra Na Pombe

  Kunywa viagra na huku unaendelea na pombe yaweza kuleta shida ya kupungua zaidi kwa presha ya damu. Kama wewe ni mnywaji wa pombe hakikisha unamjulisha daktari kuhusu hilo mapema.

  Bofya kusoma kuhusu; Kwanini unawahi kufika kileleni na kushindwa kurudia tendo

  Categories
  Hedhi salama Siku za hatari

  Kumeza P2, Maswali na Majibu

  vidonge vya p2
  vidonge vya p2 kuzuia mimba

  Nini Kinatokea P2 isipofanya kazi?

  P2 ni vidonge vya kumeza kwa dharula tu ili kuzuia mimba isiyotarajiwa endapo hukutumia kinga. Lakini unaweza kuwa unajiuliza je kuna uhakika gani kama p2 zinakusaidia kuzuia mimba? Uwezo wake ni asilimia ngapi? Na vipi kama haitafanya kazi nini kitatokea?

  Hapa chini kuna majibu ya maswali yako yote kuhusu p2 kutoka kwa watalamu na wabobezi wa afya ya uzazi. Tusome zaidi.

  Je unaweza kushika mimba hata baada ya kumeza p2?

  P2 ama morning after pill au plan B, ni dawa zilizopo kwenye kundi la levonorgestrel. Ambazo kazi yake ni kuzuia usishike mimba baada ya tendo endapo umesahau kinga, au kondomu imepasuka au ulifanya tendo ukiwa umelewa.

  Dawa zinafanya kazi kwa kuzuia yai kutolewa kwenye ovary wakati wa ovulation, na hivo kuzuia mbegu na yai zisikutane kufanye kiumbe.

  Muda sahihi wa kumeza p2 ni upi?

  Kumbuka mbegu inapoingia kwenye uke inachukua saa 12 mpaka 48 kwenda kurutubisha yai. Na dawa inafanya kazi vizuri endapo utameza ndani ya masaa 12 baada ya kufanya tendo. Ukimeza ndani ya masaa 24 chansi ya kuzuia mimba ni asilimia 95 na zaidi.

  Ukimeza kuanzia masaa 48 mpaka 72, yani siku 2 mpaka 3 baada ya kufanya tendo, chansi ya kuzuia mimba inapunguza mpaka asilimia 61 pekee. Kumbe sasa uwezekano wa kushika mimba hata kama ulimeza p2 unaongezeka kadiri unavochelewa kumeza kidonge.

  Dalili gani nitapata baada ya kumeza p2?

  Baada ya kumeza p2 tegemea kupata dalili ama side effects kama

  • kichefuchefu
  • maumivu ya tumbo
  • kichwa kuuma
  • kizunguzungu na
  • kutapika

  Kama utatapika ndani ya masaa mawili bada ya kumeza dawa, unatakiwa umeze tena kidonge kingine ama utumie njia ingine ya kuzuia mimba kama condom.

  Je uzito mkubwa na kitambi ni kikwazo cha p2 kufanya kazi?

  Jibu ni ndio, tafiti zinaonesha kwamba wanawake wenye uzito mkubwa na kitambi wapo kwenye hatari ya kushika mimba hata kama wametumia p2 vizuri. Inashauri kama wewe ni mnene tumia kitanzi cha copper kama njia ya kisasa kuzuia mimba.

  Dawa Zinapelekea P2 isifanye Kazi

  Ni muhimu pia kujua kwamba baadhi ya dawa zinaweza kuathiri utendaji wa P2. Dawa kama za fungus, HIV, dawa za kifafa na baadhi ya antibiotic,. Sasa unapoenda dukani kununua P2, hakikisha unamweleza muhudumu hali yako ya kiafya na dawa unazotumia kwa muda huo.

  Je p2 zinafanya kazi kwenye ovulation?

  Dawa za p2 zinafanya kazi vizuri kabla ya ovulation, yani kabla yai halijatolewa. Hii ni kwasababu inazuia kabisa yai kutolewa kwenye ovari na hivo kuzuia urutubishaji.

  Lakini hata kama yai limeshatolewa, kidonge kinazuia mbegu kulifikia yai, kwa kufanya ute wa ukeni uwe mzito sana kiasi mbegu zinashindwa kuogelea.

  Kama pengine umechelewa kumeza kidonge, na tayari yai limerutubishwa, basi kidonge kinazuia kiumbe kujishikiza kwenye ukuta wa kizazi na hivo mimba haitakuwepo.

  Je kuna madhara kwa mjamzito kumeza P2?

  Ni muhimu pia kujua kwamba, endapo umemeza kidonge bahati mbaya bila kujua kumbe kuna mimba, haitakuwa na madhara. Kiumbe kitaendelea kukua pasipo shida.

  Maelezo ya Mwisho Kuhusu P2

  Meza p2 kwa emergency tu na siyo kila siku. P2 ziapelekea hedhi kuvurugika na homoni kuvurugika. Tumia kwa tahadhari na usizoee kuzimeza kila siku.

  Endapo unatafuta njia ya kupanga uzazi ya mda mrefu, tafadhali tembelea hospitali uonane na muhudumu akupe maelekezo.

  Kwa ushauri zaidi na tiba tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254

  Soma hapa ikiwa hedhi yako Imevurugika na unataka kuiweka sawa.

  Categories
  Afya ya mwanamke na uzazi Hedhi salama

  Maumivu ya Tumbo la Chango

  tumbo la chango

  tumbo la chango

  Chango ni kitu gani hasa?

  Tumbo la chango au mchango, wengi husema wakimaanisha maumivu makali ya tumbo kipindi cha hedhi. Kitalamu maumivu haya huitwa dysmenorrhea, ikimaanisha maumivu kutokana na kujikaza kwa ukuta wa kizazi ili ubomoke na kutoa damu kipindi upo kwenye hedhi.

  Aina za tumbo la chango

  Kuna aina kuu mbili za maumivu haya ya hedhi ama mchango, ambayo ni primary dysmenorrhea na secondary dysmenorrhea.

  Primary Dysmenorrhea (Tumbo la Chango la kawaida)

  Chango hili la uzazi ni yale maumivu ya kawaida yanayokupata kila mwezi kwenye hedhi na hayatokani na ugonjwa wowote. Maumivu haya huanza siku moja ama mbili kabla hujapata hedhi yako. Waweza kuhisi maumivu kwenye nyonga, kiuno na tumbo pia.

  Pia chango la namna hii huchukua masaa 12 mpaka 73 yani siku 3 kuisha, na inaambatana na dalili zingine kama kichefuchefu na kutapika na hata kuharisha. Chango la namna hii huwa linapungua kadiri unazozeeka ama pale utakapozaa.

  Secondary Dysmenorrhea (Tumbo la Chango lisilo Kawaida)

  Chango lako linaposababishwa la ugonjwa fulani kwenye via vya uzazi. Chango hili huanza mapema zaidi kwenye mzunguko hata wiki kabla na inachukua mda mrefu sana kuisha. Mara nyingi chango hili halina dlaili za kuchefuchefu, kutapika kukosa nguvu na kuharisha.

  Nini kinapelekea upate maumivu makali sana kwenye hedhi?

  Maumivu hutokea pale kemikali inayoitwa prostaglandin inapofanya ukuta wa kizazi kujikaza. Ukuta wa kizazi ambapo mtoto hujishikiza na kukua,umetengenezwa kwa misuli, na unajikaza kwenye hedhi ili kubomoka kutoa damu isiyohitajika.

  Ukuta unapojikaza sana, unaleta mgandamizo kwenye mishipa ya karibu ya damu, na hivo kupunguza kiwango na hewa safi ya oksijen kwenda kwenye misuli. Na misuli inapokosa hewa ndipo unapata maumivu makali.

  Chango la uzazi kutokana na ugonjwa

  Chango hili laweza kutokea kwa kusababishwa na ugonjwa fulani, changamoto hizi ni pamoja na

  1. Endometriosis: Changamoto ambapo kuta za kizazi zinakua na kwenda nje ya kizazi. Tishu hizi nyakati za hedhi zitapelekea maumivu makali na kuvimba.
  2. Adenomysis: Hili ni tatizo ambapo kuta za kizazi zinakua kuelekea kwenue misuli ya kizazi. Tatizo hili kaweza kupelekea kizazi kutanuka na hivo kuletea bleed nyingi yenye maumvu
  3. PID: Haya ni maambukizi ya bakteria kwenye njia ya uzazi. PID yaweza kuleta maumivu makali chini ya kitovu, kwenye tendo na maumivu nyakati za hedhi yani chango.
  4. Fibroids: Hizi ni vimbe ambazo siyo za saratani ndani au nje ya kizazi, zinazopelekea chango kali sana
  5. Cervical stenosis: Hiki ni kitendo cha mlango wa kizazi kusinyaa na hivo kuzuia damu kutoka kwa kasi nzuri hivo kuleta maumivu ya chango kwenye hedhi.

  Vipimo: Utajuaje kama Chango lako la kawaida au ni hatarishi?

  Kama chango lako linachukua zaidi ya siku 3, hakikisha unaenda hospitali kufanyiwa vipimo. Kumbuka aina zote za chango zinaweza kutibiwa hospital na hata kwa tiba asili. Muhimu kwanza ni kujua nini kipo nyuma ya chango lako.

  Kwanza kabisa daktari atakwambia ujieleze dalili zote unazopata kwenye hedhi pamoja na mzunguko wako ukoje. Pili daktari atakufanyia vipimo ndani ya via vya uzazi(pelvic exam) ambapo ataingiza kifaa ukeni kucheki kama kuna hali yoyote isiyo ya kawaida kwenye uke, mlango wa kizazi na kizazi chenyewe.

  Daktari anaweza pia kuchukua kiwango cha majimaji kwenye uke na kupeleka maabara kwa ajili ya vipimo zaidi.

  Nini kinatokea kama kuna ugonjwa?

  Kama daktari atahisi pengine kutokana na dalili zako una chango la ugonjwa, hapo utafanyiwa utrasound. Na ikionekana kuna shida, daktari atajikita zaidi kukutibu tatizo husika.

  Nini cha Kufanya ili Kupunguza Maumivu ya Chango kwa Muda

  Kuna njia nyingi ambazo husaidia kupunguza maumivu ya hedhi ambazo unaweza kutumia ukiwa nyumbani kwako kabla ya kwenda hospitali. Kama maumivu ni makali sana unaweza:-

  • Kumeza dawa za kukata maumivu kama ibuprofen kwa ahueni ya haraka. Angalizo: dawa za maumivu isiwe ni nia ya kutumika kila mara kwani madhara yake ni makubwa kiafya, dawa hizi zitumike kwa uangalifu.
  • Tumia maji ya uvuguvugu kukandakanda mahali pa tumbo la chini
  • Epuka kuvuta sigara na kunywa pombe kipindi cha hedhi
  • Usitumie vinywaji na vyakula vyenye caffeine mfano majani ya chai na kahawa
  • Fanya masaji kwenye upande wa chini wa mgongo na sehemu ya tumbo la chini.
  • Pata muda mwingi wa kupumzika
  • Weka ratiba ya kufanya mazoezi mara kwa mara: Tafiti zinasema wanawake wanaofanya mazoezi hupunguza maumivu ya hedhi kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na wasiofanya mazoezi.

  Lini natakiwa Kumwona Daktari?

  Chango linapokuwa kali sana linapelekea baadhi ya wanawake washindwe kufanya kazi zao na kushindwa kwenda darasani. Huhitaji kabisa kuvumilia mateso ya namna hii, unahitaji kuishi vizuri na kufurahia maisha. Kama maumivu hayavumiliki hakikisha unaenda hospital haraka.

  Jua mzunguko wako

  Ni muhimu sana kujua mzunguko wako, pia ujue maumivu huwa yanaanza siku ngapi kabla ya hedhi. Kama chango linaambatana na dalili zingine mfano maumivu makali ya kichwa, bleed nzito sana na nyingi, nenda hospitali.

  Je Tumbo la Chango Linapelekea Ugumba?

  Kama tulivoona kwamba chango siyo ugonjwa bali ni dalili za maumivu makali ya tumbo la hedhi. Sasa kama unapata chango la kwanza (primary amenorrhea) hapo hakuna kikwazo cha kushika mimba. Lakini kama chango lako ni ile aina ya pili yani secondary amenorrhea, hapo lazima kuwe na kikwazo kushika mimba mapema.

  nini ufanye kama umetafuta mimba mda mrefu bila mafanikio?

  Endapo wewe na mme wako mmetafuta mimba kwa zaidi ya mwaka mmoja, nendeni hospitali wote wawili kupimwa kujua chanzo cha tatizo. Mwanamke utapima mirija, kizazi na homoni na mwanaume atapimwa mbegu kuona kama zina hitilafu.

  Unahitaji ushauri na tiba? Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254