Categories
Afya ya mwanamke na uzazi

Kupona Mapema Baada Ya Kujifungua Kwa Upasuaji

Kujifungua mtoto ni jambo la furaha sana kwa kila mwanmke aliyekuwa mjamzito. Maana mwisho wa siku unapata kiumbe chako baada ya kukibeba tumboni kwa shida miezi tisa yote. Kujifungua kwa uke kuna tofauti na kujifungua kwa upasuaji.

Pamoja na furaha yote lakini kumbuka kwamba kujifungua kunakuja na mzigo mwingine hasa mabadiliko ya mwili wako. Shepu itabadilika sana na utahitaji kuzoea tabia mpya. Kama umejifungua kwa upasuaji utahitaji mda nwingi zaidi wa kupumzika. Hapa chini ni

Hatua za tano za kukusaidia kupona mapema baada ya kujifungua kwa upasuaji

1.Pata Muda Zaidi Wa Kupumzika

Kama ilivyo kwa upasuaji mwingine, upasuaji wa kujifungua unataka upumzike zaidi ili kupona mapema. Baada ya kujifungua unaweza kukaa hospitali kwa siku 3 mpaka 5, na baada ya hapo itachukua mpaka week 6 kupona kabisa.

Hakikisha unalala kila wakati mtoto anapopata usingizi, maana akiamka atahitaji uwepo wako. Pata usaidizi kutoka kwa ndugu ama uwe na mfanyakazi(beki tatu) kwa ajili ya kumbeba mtoto na kubadilisha nguo, itakusaidia kupumzika zaidi

2.Usifanye Kazi Ngumu

Unapojifungua kwa upasuaji mwili unalegea na wahitaji matunzo kama ya mtoto mdogo. Usipandishe ngazi wala kuinua vitu vizito sana. Hakikisha kila kitu inachohitaji kwa haraka kama nepi, pampasi na chakula kipokaribu yako.

Usibebe kitu chochote kizito zaidi ya mtoto wako. Waambie ndugu wa karibu wakusaidie kubeba maji kupeleka bafuni na vitu vingine vizito. Unapotaka kukohoa au kupiga chanya basi hakikisha unashikilia tumbo lako ili kuulinda mshono.

Ongea na daktari akujulishe ni baada ya muda gani utaruusiwa kuanza kazi zako na pia mazoezi ili kutengeneza tena shepu yako.

3.Usianze mazoezi magumu haraka

Fanya mazoezi mepesi, kama kutembea kila siku kadiri utakavoweza. Pia usianze kufanya tendo mapema, subiri mpaka pale daktari atakapokuruhusu.

Usisahau pia kuwa makini na afya ya akili kama vile unavotunza mwili wako, tunza na hisia zako pia. Kuwa na mtoto mchanga itakupa hisia mbalimbali ikiwemo hasira za hapa na pale, uchovu na zingine. Zungumza na rafiki yako wa karibu namna unavojisikia au mshauri wa afya ya akili.

4.Tumia dawa za Maumivu inapobidi

Ongea na daktari kabla ya kumeza dawa pale maumivu yanapokuwa makali sana. Kumeza dawa kiholela kwa kipidi hii unaponyonyesha ni hatari.

Pata Lishe Ya Kutosha

Mlo kamili ni muhimu sana kwa kipindi hiki unaponyonyesha na unapouguza kidonda chako. Kumbuka kwamba mtoto wako anategemea sana chakula unachokula.

Hakikisha unakula aina nyingi za vyakula katika siku husika. Tafiti zinasema kwamba kutumia mboga za majani kwa wingi wakati wa kunyonyesha zinafanya ladha ya maziwa kwa mtoto kuwa nzuri na mtoto ufurahia zaidi anaponyonya. Pia muhimu kunywa maji ya kutosha ili usipate choo kigumu ama kukosa choo.

Lini Watakiwa Kumwona Daktari?

Wakati unajiuguza unaweza kupata hali ya kidonda kupata malengelenge na damu kutoa kidogo hiyo ni kawaida. Lakini ukiona dalili hizi hapa chini hakikisha unaenda hospitali haraka.

Dalili mbaya ni pamoja na

 • kidonda kuwa chekundu, kuvimba na kutoa usaha
 • maumivu makali sana eneo la kidonda
 • homa kali ya zaidi ya nyuzijoto 38
 • kutokwa na uchafu wenye harufu kali ukeni
 • kutokwa na damu nyingi ukeni
 • miguu kuvimba
 • kushindwa kupumua vizuri
 • maumivu ya kifua
 • maumivu kwenye eneo la matiti

Kama kuna ndugu au rafiki yako aliwahi kujifungua kwa upasuaji usijilinganishe nae katoka kupona kwako. Kila mwanamke ana mwili wa tofauti, wekeza nguvu na hisia zako katika afya yako itakusaidia kupona mapema.

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu: Maandalizi ya kujifungua kwa upasuaji

Categories
Afya ya mwanamke na uzazi

Kipimo cha Mimba na Jinsi ya Kusoma Majibu

kipimo cha mimba
UPT

Jinsi Gani Kipimo Cha Mimba Kinafanya Kazi?

Kipimo cha mimba kinafanywa kwa kuchukua sampuli ya mkojo au damu ili kupima uwepo wa homoni inayoitwa human chorionic gonatrophin(hCG). Mwili wako huanza kuzalisha homoni hii baada tu ya yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye ukuta wa kizazi. Kiwango cha kuzalishwa homoni hii huongezeka na kudabo kila baada ya siku 2 mpaka3.

Aina za Vipimo vya Mimba Zinazotumika Mara kwa Mara

Kipimo cha Damu

Kinafanyika hospitali pekee, hakitumiki sana kama kile cha mkojo, na majibu yake huchukua muda zaidi, yahitaji kusubiri. Kipimo hichi kinaweza kugundua uwepo wa mimba katika kipindi kifupi sana baada ya kushika ujauzito kabla hata hujaanza kuona dalili, ndani ya siku 6 mpaka nane.

Kipimo Cha Mkojo

UPT ama kipimo cha mkojo waweza kufanya ukiwa nyumbani ama hospitali. Unaweza kununua kifaa cha kupima famasi ya karibu ukapima na kujua majibu pasipo mtu mwingine yeyote kufahamu. Ni kipimo rahisi kutumia na kinatoa majibu haraka sana.

Maandalizi ya kufanya kipimo cha mimba cha mkojo

Kama unafanya kipimo ukiwa nyumabni, zingatia yafuatayo

 • hakikisha unasoma kwa uangalifu maelekezo ya matumizi, kwenye pakiti lenye kifaa cha kupimia kabla hujaanda mkojo wa kupima
 • Hakikisha kipimo hakijaexpire
 • Pima mkojo wa kwanza wa asubuhi baada ya kupitisha hedhi yako
 • Usinywe maji au kinywaji chochote kwa wingi, kwasababu itafanya homoni ya HCG kuwa kidogo na kutoonekana kwenye kipimo.

Namna ya kupima ni kwa kukusanya mkojo kiasi kidogo kwenye kikombe, kisha unazamisha kipimo kwa muda wa dakika 5. Ili kupata uhakika zaidi unaweza kwenda hospitali pia ukaonana na daktari akakupima zaidi.

Endapo hujaridhika na majibu yako, subiri tena week moja kisha upime kwa usahihi kama ulivoelekezwa na mtoa huduma alieykuuzia kifaa. Pia unaweza kwena hospitali na kufanya kipimo cha damu. Kipimo cha damu kinaweza kugundua mimba hata ndani ya week moja tu.

Kipimo cha Mimba ni sahihi Kwa asilimia Ngapi?

Maarufu kama UPT kipimo hiki waweza kufanya ukiwa nyumbani kinaweza kukupa usahihi wa matokeo kwa ailimia 99, kama utafuata maelekezo vizuri ya upimaji. Kipimo cha damu ni sahihi zaidi ya asilimia 99. Kumbuka usahihi wa kipimo kama umejipima mwenyewe nyumbani unategemea jinsi gani umefuata maelekezo ya kupima na umri wa ujauzito

Lini Unatakiwa Kufanya Kipimo cha Mimba?

Baadhi ya vipimo vya homoni ya HCG vinaweza kutoa matokeo hata kabla ya kukosa hedhi yaani week moja baada ya kushika mimba, lakini fahamu kwamba matokeo yatakuwa sahihi zaidi endapo utasubiri mpaka ukose hedhi inayofuata.

Nawezaje Kupata Kipimo cha mimba nijipime Nikiwa Nyumbani?

Unaweza kununua famasi ya karibu na ukapata maelekezo kutoka kwa muhudumu wa famasi namna ya kutumia. Ni bei ndogo tu sh elfu moja.

Majibu ya Kipimo Yanasomwaje?

Vipimo vingi kama mimba ipo huonesha mistari miwili ya rangi nyekundu na mstari mmoja kama hakuna mimba. Baadhi ya vipimo huonesha alama ya chanya(+) na vingine huandika neno pregant au not pregnant.

Kwa ushauri zaidi, tuandikie whatsapp kwa namba 0678626254. Usituandikie kuomba ushauri wa kutoa mimba, hatutakujibu.

Bofya makala inayofuata: Dalili za mimba lakini kipimo kinasoma negative

Categories
Uzazi wa Mpango

Je Kitanzi ni Njia Salama Kupanga Uzazi?

Jinsi ya kutumia Kitanzi
kitanzi

Kama wewe ni mwanamke unayetafuta njia gani salama ya kutumia upange uzazi wako, basi bilashaka umewaza kuhusu njia ya kitanzi. Kitanzi ni njia salama kwa wanawake wengi sana kwa sasa japo siyo wote.

Wengi inawakaubali na haina madhara makubwa ukilinganisha na njia zingine kama njiti, vidonge na sindano.

Kitanzi ni Nini

Kitanzi ama intrauterine device ni kifaa chenye umbo la T kinachoingizwa kwenye kizazi cha mwanamke ili kuzuia mimba isitunge kwa kuzuia mbegu ya kiume isilifikie yai lililokomaa na kulirutubisha. Kitanzi kikitumika ipasavyo uwezo wake wa kuzuia mimba ni zaidi ya asilimia 99.

Ni zipi faida za Kutumia Kitanzi?

 • kinaweza kutumika kwa muda mrefu bila kubadilisha
 • huhitaji kukagua ama kufatilia mara kwa mara, ukishaweka mara moja tu kwa usahihi inatosha
 • gharama yake ni nafuu na unalipia mara moja tu
 • ni salama kutumia hata kama unanyonyesha

Ni watu gani wanapaswa kutumia kitanzi?

Wanawake wote wenye afya njema wanaweza kutumia kitanzi. Ila kumbuka kitanzi hakizuii kutoambukizwa magonjwa ya zinaa. Usitumie kitanzi kama

 • unaugua ugonjwa wa zinaa ama umeugua PID hivi karibuni
 • ni mjamzito
 • una saratani ya kizazi au ya shingo ya kizazi
 • una tatizo la kutokwa damu kusiko kawaida

Je hedhi yangu itabadilika baada ya kuweka kitanzi?

Baadhi ya wanawake hupata maumivu kiasi kwenye hedhi baada ya kuweka kitanzi na hedhi kuwa nzito sana. Kwa miezi michache ya mwanzoni baadhi wanaweza kuona hedhi ikivurugika. Wanawake wengi hupata hedhi kidogo ama wengine hukosa kabisa hedhi.

Je Mwanaume Atakigusa Kitanzi Wakati wa Tendo la ndoa?

Kama kitanzi kimewekwa vizuri basi mwanaume ni ngumu kugusa kitanzi wakati wa tendo. Lakini hata kama ikitokea hivo basi haiwezi kupunguza ladha ya penzi kwasababu pia kamba fupi za kitanzi zinazobaki nje ya uke huendelea kuwa laini zaidi kadiri muda unavoenda.

Je kuna Madhara ya Kutumia kitanzi?

Kitanzi ni njia salama zaidi ya kisasa kupanga uzazi. Wanawake wengi hupata madhara madogo madogo ya kawaida kama kizunguzungu ambayo huisha ndani ya muda mfupi. Mwanzoni unapoweka kitanzi tegemea kupata maumivu kama vile yale ya hedhi.

Kama unapata maumivu makali sana ya tumbo ama kutokwa damu, tembelea hospitali mapema kupata ushauri wa dakari

Mmoja kati ya wanawake kumi waliowekewa kitanzi anaweza kupata vimbe ndogo ndogo kwenye mayai(ovarian cyst). Kwa kisi kikubwa vimbe hizi hazina madhara na huisha zenyewe bia dawa.

Kama utapata dalili za tumbo kujaa, kuvimba na maumivu makali chini ya kitovu muhimu uende hospitali haraka.
Kwa kiasi fuani matumizi ya kitanzi huongeza hatari ya kuugua PID, ambayo ni maambukizi kwenye kizazi, mirija na mifuko ya mayai.

Dalili za PID ikiwa ni pamoja na maumivu wakati wa tendo, kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya ukeni, hedhi nzito kupita kiasi na homa. Muone daktari mapema kama unaanza kupata dalili hizi ili utibiwe na kuepusha madhara zaidi ikiwemo kuziba kwa mirija.

Je kitanzi kinaweza kutoka chenyewe ?

Daktari atakuchunguza kama kitanzi hakipo sawa kila mara unapotembelea hospitali. Kitanzi kinatakiwa kishikiliwe na shingo ya kizazi. Kwa baadhi ya wanawake kitanzi kinaweza kutoka nje ya kizazi.

Hali hii hutokea hasa kama

 • hujawahi kuzaa
 • una umri chini ya miaka 20
 • umewekewa kitanzi mapema sana baada tu ya kuzaa au baada ya mimba kuharibika
 • una vimbe(fibroids) kwenye kizazi
 • kizazi chako kimeinama ama kina shape isiyo ya kawaida

Je vipi kama Nahitaji kuzaa kwa siku za baadae?

Kutumia kitanzi kwa watu wengi haitaathiri uwezo wako wa kushika mimba siku za baadae. Kama utafikia wakati unahitaji kubeba mimba ingine, tembelea hospitali onana na daktari muombe akutolee kitanzi. Baada ya hapo hedhi yako itarudi kuwa kawaida na utashika mimba mapema.

Je vipi kama sitashika mimba mapema?

Inatokea kwa wanawake wachache kupata madhara ya kitanzi, hasa kuvurugika kwa mazingira ya kizazi na hivo mimba kutoshika. Kwa grupu hili la wanawake tunawashauri kutumia hizi tiba asili ili kusfaisha kizazi na kusaidia mayai kupevuka. Asilimia 90 ya wanawake tuliowapa dawa hizi walishika mimba ndani ya miezi miwili.

Jaribu dawa hizi endapo umekwama kushika mimba mapema baada ya kutoa kitanzi, bofya hapa.

Kwa ushauri zaidi, tuandikie whatsapp kwa namba 0678626254.

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu kupandikiza mimba

Categories
Afya ya mwanamke na uzazi Siku za hatari

Je Unaweza Kushika Mimba Kwenye Hedhi?

kushika mimba kwenye hedhi
Upt

Endapo unatafuta mimba kwa muda mrefu bila mafanikio au unataka kushika mimba haraka, ni muhimu kufatilia kwa makini mzunguko wako wa hedhi kujua zipi siku za hatari. Moja ya imani potofu sana kwa wengi ni kuamini mwanamke hawezi kushika mimba kwenye hedhi.

Japo uwezekano ni mdogo wa kushika mimba wakati wa hedhi lakini inawezekana. Hapa chini ni maelezo ya kina unayotakiwa kufahamu kuhusu kufanya tendo na kushika mimba wakati wa hedhi.

Mimba inatungwaje?

Mchakato wa kushika mimba kwa mwanamke ni moja ya maajabu makubwa sana ya uumbaji wa binadamu. Yahitaji mbegu kutoka kwa mwanaume iungane na yai kutoka kwa mwanamke.

Yai likishapevuka na kutolewa kutoka kwenye mfumo wa mayai, linaweza kushi kwa masaa 12 mpaka 48 kabla ya kuharibika. Mbegu ya amwanaume ikishatolewa inaweza kuishi ndani ya kizazi cha mwanamke kwa siku mpaka tatu mpaka tano.

Siku za hatari

Wanawake wengi hupata hedhi kila baada ya siku 28 mpaka 33 za mzunguko. Na wengi wao mayai hukomaa siku ya 14 baada ya hedhi . Siku yai kutolewa inaweza pia kuwa ya 12, 13 14 au 15, siku hizi ndizo tunaziita siku za hatari.

Kitendo cha yai kupevuka na kutolewa kwa ajili ya urutubishaji huitwa ovulation. Na endapo kama yai na mbegu vitakutana basi uwe na uhakika mimba itatungwa.

Nini kinapelekea kushika mimba kwenye hedhi?

Siku ya yai kupevuka na kutolewa inatofautiana kulingana na mzunguko wako. Baadhi ya wanawake wenye mzunguko mrefu wa siku mpaka 35, ovulation yaweza kutokea siku ya 21 . Na wanawake wenye mzunguko mfupi zaidi wanaweza kushika mimba hata siku ya 7 ya hedhi.

Sasa kwa mantiki hii, chukulia hedhi yako inachukua siku 6 kuisha. Umefanya mapenzi na mtu katika siku ya tano ya hedhi, na yai ikapevuka siku ya 7, na tunajua mbegu zinaweza kukaa siku mpaka 6 ndani ya kizazi. Maana yake unaweza ukashika mimba ukikutana na mwanaume kwenye siku za hedhi yako.

Sababu ingine ni kuchanganya bleed ya ovulation na bleed ya hedhi.

Wakati wa ovulation mwanamke anaweza kupata matone kidogo ya damu kwa siku moja . Wanawake wengi waaweza kuhisi ni damu ya hedhi. Kufanya tendo bila kinga katika muda huu utaweza kushika mimba.

Kama unahitaji kufatilia vizuri kujua siku zako za hatari, anza kwa kuweka rekodi ya mizunguko yako ya hedhi kwa miezi walau mi4. Andika lini unaanza hedhi, unamaliza baada ya muda gani, hedhi yako ikoje?.
Ukifatilia kwa miezi kadhaa ni rahisi kujua siku zako za hatari na ukaweza kucheza salama.

Uwezekano ukoje wa kushika mimba kwenye hedhi?

Chansi ya kushika mimba kwa mwanamke unaongezeka na kupungua kulingana na mwenendo wa siku zako za yai kupevuka. Uwezekano wa kushika mimba siku ya kwanza na ya pili ya hedhi ni mdogo sana chini ya asilimia 1.

Baada ya kuanza hedhi kwenye siku ya 13 uwezekano wa kushika mimba ni karibu asilimia 9 na chansi kuongezeka zaidi siku ya ovulation.

Tumia uzazi wa mpango kuepuka kushika mimba kwenye hedhi

Endapo bado hujajiandaa kabisa kushika mimba unaweza kuamua kutumia uzazi wa mpango. Nenda hospitali, onana na daktari atakupa maelekezo ya njia zote zinazotikana ikiwemo faida na hasara za kila njia ya kupanga uzazi.

Baada ya maelezo ya daktari, utaweza kuchagua njia sahihi ya kutumia itakayokufaa ili kuzuia kushika mimba kwenye hedhi. Kumbuka tu kwamba njia nyingi za uzazi wa mpango haziwezi kukuzuia kupata magonjwa ya zinaa.

Zitakukinga tu dhidi ya miba isiyotarajiwa. Kama huna uhakika na mwenzi wako, hakikisha unatumia kinga kama kondomu, itakusaidia kukukukinga na magonjwa ya zinaa na mimba pia.

Hitimisho

Mzunguko wa hedhi unatofautiana kwa kila mwanamke, hivo inawezekana kabisa ukashika mimba siku za hedhi. Japo chansi ya kushika mimba ni ndogo mwanzoni mwa hedhi ila kadiiri unavokarbia siku ya ovulation chansi inaongezeka.

Kama umeshajaribu kutafuta mimba kwa zaidi ya mwaka mmoja bila mafanikio, muone daktari kupata vipimo na tiba. Daktari anaweza kukwelekeza vizuri namna ya kufatilia siku za hatari ili ushike mimba mapema.
Daktari pia anaweza kukufanyia vipimo kadhaa na kukupa dawa za kuchochea upevushaji wa mayai na kuongeza chansi ya kushika mimba.

Kwa ushauri zaidi, tuandikie whatsapp kwa namba 0678626254.

Bofya kusoma makala inayofuata: Jinsi ya kugundua siku za hatari kushika mimba

Categories
Tendo la ndoa

Tendo la Ndoa wakati wa Ujauzito

tendo la ndoa wakati wa ujauzito
mjamzito

Kama mwanamke unaweza kuwa unanjiuliza kama ni salama kufanya tendo la ndoa wakati wa ujauzito ama siyo salama.

Pengine unafikiri yaweza kupekea mimba kuharibika? Au mtoto kupata majeraha? Pengine wajiuliza kuna staili fulani za tendo ambazo ni salama zaidi kwa mjamzito? Hapa chini ni taarifa muhimu ambazo watakiwa kuzifahamu.

Je Kufanya Tendo la Ndoa Wakati wa Ujamzito Ni Salama?

Jibu ni ndio, kufanya tendo wakati wa ujauzito ni salama kabisa. Uume kuingia ndani ya uke,zile pilika za kuingiza na kutoa haziwezi kuathiri mtoto, kwa sababu analindwa na tumbo na misuli ya ukuta wa kizazi pia.

Lakini pia mtoto analindwa na majimaji mazito(amniotic fluid).
Usijali kuhusu kusinyaa na kutanuka kwa uke pale unapofikia kilele, hakuwezi kufanya mimba ikatoka. Kutanuka huku ni tofauti na wakati wa kuzaa.

Mazingira gani inashauriwa usifanye tendo la ndoa wakati wa ujauzito?

Daktari anaweza kushauri usifanye tendo la ndoa kama

 • una historia ya mimba kuharibika mara kwa mara
 • uko kwenye hatari ya kupata uchungu mapema kabla ya week 37 za ujauzito
 • unatokwa na damu na maumivu yasijulikana sababu yake
 • chupa imepasuka na maji yanavuja
 • mlango wa kizazi umefunguka mapema zaidi
 • una tatizo kitaalamu placenta previa yani tishu za mirija unaomlisha mtoto chakula na hewa safi, umekuwa mpaka kuziba mlango wa kizazi
 • kama unatarajia kujifungua watoto mapacha

Je naruhusiwa kupiga punyeto badala ya tendo?

Fahamu kwamba daktari akishauri usifanye tendo anamanisha pia usifanye kitu chochote ambacho kinakuamsha hisia na kukufikisha kileleni mfano kutumia dildo an vidole/ kupiga punyeto.

Hamu ya Tendo la Ndoa wakati wa Ujauzito

Kila mwanamke mwanamke mjamzito anatofautiana namna anavojisikia kuhusu tendo. Baadhi hamu ya tendo hupotea kabisa. Wengine hufurahia zaidi tendo na kupata msisimko zaidi wa mapenzi wakati huu.

Kipindi cha ujauzito ni kawaida kwa hamu ya tendo kubadilika. Muhimu zungumza na mpenzi wako namna unavojisikia. Mueleze unapenda staili ipi nzuri ya kufanya tendo isiyokuumiza.

Staili za Kufanya Tendo Kwa Mjamzito

Baada ya miezi minne ya mimba,usifanye tendo kwa njia ya kawaida ya baba na mama kwa kulala kitandani na mme wako akaja kwa juu. Itakusaidia kuepuka changamoto za mzunguko wa damu..

Staili nzuri ya kufanya tendo ni kwa wote kulala kwa ubavu. Kisha mwanaume akaingiza uume kwenye uke kupitia nyuma yako na pia dogie style,yani mwanamke kupiga magoti na mwanamume kuingiza uume kwa nyuma.

Kama huna uhakika na mwanaume unayekutana nae kipindi hiki cha ujauzito basi hakikisha anavaa kondomu. Kuwa na mimba haizuii kutoambukizwa magonjwa ya zinaa kama ukimwi, kisonono na chlamydia-maana maambukizi haya huathiri mtoto moja kwa moja.

Tendo la Ndoa Baada Ya Kujifungua

Kwa week 6 za mwanzo baada ya kujifungua inashauriwa usifanye tendo la ndoa. Sababu zikiwa unahitaji:-

 • kupona kidonda wendapo njia ya uke ilikatwa kidogo kuongeza mlango wa mtoto kutoka
 • kupona kidonda cha tumbo endapo kama ulijifungua kwa upasuaji
 • uchovu kutokana na kujifungua
 • mabadiliko ya homoni yatapelekea ukose hamu ya tendo kwa muda
 • baaada ya kuzaa ni kawaida kuendelea kupata bleed kwa week 4 mpaka 6
 • Stress kutokana na kuwaza sana kuhusu majukumu mapya kama mzazi

Kwa ujumla tendo la ndoa lifanyike baada ya mama kupona kabisa. Ongea na daktari wako akupe ushauri lini itakuwa sawa. Kwa kiasi kikubwa week 6 zinafaa kusubiri kabla ya kuanza tena tendo la ndoa. Muhimu hakikisha tu una utulivu kihisia na kimwili kabla ya kuanza .

Bofya kusoma makala inayofuata: Bawasili kwa mjamzito, Ushauri na tiba