Maumivu ya tumbo yanaweza kusababishwa na vitu vingi sana na yanaweza kuhusisha zaidi ya kiungo kimoja cha mwili. Na maumivu ya tumbo chini ya kitovu yanahusisha viungo vyote vya uzazi, na viungo vingine kama figo na kibofu. Maumivu yanapoanza inaweza kuwa ngumu kujua chanzo cha tatizo ndiomaana ni muhimu kwenda hospital.
Nini kinapelekea maumivu ya Tumbo chini ya kitovu?
Maumivu chini ya kitovu yanakuja kutokana na athari kwenye viungo vya karibu. Viungo hivi ni pamoja na
- utumbo mdogo
- utumbo mkubwa
- kizazi
- mifuko ya mayai
- kibofu cha mkojo
- mirija ya kubeba mkojo kutoka kwenye figo mpaka kibofu na
- Nyonga
Mara chache inaweza kutokea athari ikaanzia viungo vya mbali kabisa, lakini maumivu yakasafirishwa mpaka eneo la chini ya kitovu. Wakati ukipata hitilafu kwenye figo, figo zipo eneo la juu na maumivu yake yaweza kusambaa mpaka chini ya kitovu. Pia kama korodani zako zinauma maumivu yanaweza kusambaa mpaka chini ya kitovu
Aina za maumivu ya tumbo chini ya kitovu
Maumivu ya tumbo yanaweza kuwa ya muda mfupi ama ya mda mrefu. Maumivu ya mda mfupi yanaweza kusababishwa na jeraha au maambukizi kwenye kiungo husika. Magonjwa makubwa yanaweza kupelekea maumivu ya mda mrefu. Muone daktari mapema endapo maumivu yako yanaongezeka kila siku na hayaishi.
Je maumivu ya tumbo chini ya kitovu ni tatizo kubwa?
Kama tulivoona hapo juu, maumivu ni kiashiria kwamba kuna tatizo fulani la kiafya kwenye mwili. Ni ngumu kutambua chanzo kwa kufatilia maumivu pekee. Ni muhimu kumwona daktari akupime kugundua chanzo cha tatizo. Daktari atakupa dawa za kupunguza maumivu wakati huo atashugulika kujua chanzo.
Nini chanzo kikubwa cha maumivu ya tumbo chini ya kitovu?
Viungo kama utumbo mkubwa na mdogo vipo eneo la tumbo la chini, na vinachukua nafasi kubwa sana pale. Kwa sababu hiyo changamoto yoyote inayoathiri utumbo basi yaweza kuwa chanzo cha maumivu chini ya kitovu.
Changamoto hizi za kila siku ni pamoja na
- gesi tumboni
- chakula kutosagwa vizuri
- kuharisha na
- kukosa choo na choo kigumu
Kama chakula hakisagwi vizuri na tumbo kujaa, waweza kuwa na aleji na aina fulani ya chakula, ama tumbo lako haliwezi kusaga aina fulani cha chakula. Suluhisho ni kuacha kabisa kutumia aina ya chakula ambacho unaona mwili umekikataa.
Pia yawezekana utumbo umebimba kwa ndani. Magonjwa yanayopelekea utumbo kuvimba ni pamoja na
- vudonda vya tumbo
- maambukizi ya bakteria
- Celiac disease (ambapo mwili unashambulia kiambata cha guleten ambacho hupatikana kwenye ngano)
- Majeraha kwenye utumbo mdogo na mpana na
- Saratani kwenye utumbo
Je nini chanzo cha maumivu ya tumbo kwa mwanamke?
Kama wewe ni mwanamke, viungo vya uzazi vipo eneo la chini ya kitovu. Viungo hivi ni chanzo kingine kikubwa cha maumivu ya tumbo chini ya kitovu. Japo maumivu ya tumbo la hedhi ni kawaida kwa kila mwanamke, sometime yanaweza kuashiria uwepo wa changamoto flani ya kiafya kama
- PID
- Vimbe kwenye kizazi (fibroids)
- Kizazi kututumka (endometriosis)
- Saratani ya kizazi
- Vimbe kwenye mayai
Magonjwa ya Figo
Kama tatizo siyo kwenye mfumo wa chakula, basi yawezekana kuna shida kwenye njia ya mkojo ambako figo zinahusika. Ugonjwa mkubwa kwenye njia ya mkojo ni UTI yani maambukizi ya bakteria kwenye njia ya mkojo. UTI inaweza kuathiri kibofu cha mojo, mirija ya kusafirisha mkojo na hata figo pia. Na matatizo yote haya huzalisha maumivu kwenye kitovu.
Vipi kama maumivu ya tumbo yanatokea upande wa kushoto au kulia?
Maumivu ya tumbo upande wa kushoto chini ya kitovu yanaweza kutokana na athari kwenye utumbo mpana. Yawezekana kukawa na bakteria waliojificha eneo hilo na kupelekea kututumka mpaka kuleta maumivu.
Maumivu yakiwa eneo la chini kulia, yaweza kuwa ni appendix. Hiki ni kifuko kidogo ambacho huhifadhi mawe. Kifuko kinaweza kushambuliwa na bakteria ama kikajaa uchafu na hivo suluhishi ikawa ni kukiondoa kabisa.
Pia Maumivu kulia na kushoto kwa chini inaweza kutokana na athari kwenye mifuko ya mayai ama figo. Uvimbe kwenye yaia au mawez kwenye figo vyote hupelekea upate maumivu. Pia kama yai linatolewa kwenye kikonyo siku ya hatari, laweza kupelekea maumivu haya.
Je lini natakiwa kumwona daktari?
Muone daktari haraka sana kama
- Maumimvu yamekuja haraka na ni makali sana
- Maumivu yanazidi kuwa makali siku hadi siku
- umeshindwa kwenda haja ndogo au kubwa kwa siku kadhaa
- unapata dalili za unjano kwenye macho
- unapata homa kali, kichefuchefu na kutapika
- Tumbo lako ni gumu au laini sana ukishika
- ulipata ajali hivi karibuni na maumivu yameendelea
- una mimba